,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 21, 2016

Muziki wa Singeli ni muziki ambao unakua kwa kasi sana kwasasa, kias kwamba hata wasanii wengine ambao hawakuwa wakifanya muziki huo hapo awali wamekuwa wakiuangalia kwa jicho lingine kabisa muziki huo. Na baadhi yao tumeanza kuwaona wakitaka kujikita katika muziki huo.Lakini huwezi kutaja Singeli halafu ukaacha kuwataja wasanii Sholo Mwamba na Man Fongo. Kwasababu hao ndio wasanii ambao wameupigania muziki huo na kuufanya hadi sasa unaeleweka kutokana na kazi zao nzuri na vitu kama hivyo.
Lakini cha kushangaza ni kwamba wawili hao hivi sasa hawana maelewano mazuri, na kisichofahamika ni kwamba ni kiki za kibiashara ili kuhakikisha bifu hilo linaupa faida muziki wao au ni matatizo yao binafsi, sote hatuna uhakika juu ya hilo ispokuwa wao wawili.Mwanadada Snura ameonekana kuwa mkereketwa wa bifu hilo kiasi kwamba ameamua kutumia ukurasa wake wa instagram kwa kuonyesha hisia zake jinsi gani amemiss ukaribu wa wawili hao.


Na kuandika caption ambayo inalenga kuutamani uelewano wa wawili hao, na kuwapa ujumbe mzito kuwa“Wote tunatafuta na wala hakuna mkamilifu.”
Wewe kama mdau wa muziki unalizungumziaje hili bifu la wasanii Man Fongo na Sholo Mwamba? Tuachie maoni yako hapa chini kwenye uwanja wa comments.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi