,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 28, 2016

Rapa mkongwe Tanzania Soggy Doggy amefunguka na kusema kuwa vijana kwenye muziki wa hip hop saizi wanafanya vizuri na ili uende nao sawa lazima upite njia wanazopita wao.

Hii inamfanya hata yeye ameshindwa kuachia kazi mpya mpaka akamilishe video kabisa, Soggy Doggy akiwa katika Planet Bongo iliyokuwa ikiruka mubashara kutoka Mabibo, Jijini Dar es Salaam.
Soggy Doggy alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho jana kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutoka Mabibo Mwisho Jijini Dar es Salaam,
Soggy anasema kwa wasanii wa hip hop sasa akimsikiliza rapa Country Boy ni kama anamsikiliza marehemu Albert Mangwea.
Ngwea%20_0
Ngwea & Country Boy
Alisema“Vijana saizi wanafanya poa sana ndiyo maana na mimi nataka niende nao sawa, sitaachia kazi mpya sasa mpaka nione nimekamilisha video kali kabisa ila kazi zipo nyingi sana ndani.
Aliendelea “ila kuna huyu mtoto Country Boy ninapomsikia katika kazi zake ni kama namsikiliza Albert Mangwea” alisema Soggy Doggy

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi