,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 21, 2016

img_9995
Muigizaji na Mkurugenzi wa kampuni ya Ndauka Advert Limited, Rose Ndauka ameitambulisha rasmi label yake itakayowasimamia wasanii wa Bongo Fleva ‘Ndauka Music’ pamoja na kumtambulisha msanii wake mpya, Kassim Casso aka Casso mbele ya waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Ndauka amesema kuwa ni muda mrefu amekuwa akitamani kusaidia vijana wenye vipaji.
“Kwa muda mrefu nilikuwa natamani kuwasaidia vijana wenye vipaji, takribani mwaka mmoja au miwili iliyopita tulianza kuifanya kazi hiyo mimi pamoja na menejimenti nzima ya Ndauka Advert. Kwahiyo leo tunaannounce lebo ya Ndauka Music pamoja na kumtangaza msanii wetu wa kwanza anaitwa Casso pamoja na kutambulisha wimbo wake mpya ‘Kitonga’. Kuna mengi yanakuja kupitia Ndauka Music chini ya Ndauka Adverts,” amesema Ndauka.
Mkurugenzi huyo alieleza pia sababu ya kuingia kwenye muziki na si kuibua vipaji vya wasanii wa filamu huku soko lake likionekana kutofanya vizuri.
“Mimi kama muigizaji naamini sanaa inagusa sehemu kubwa, nikiongelea Ndauka Adverts chini yake kuna Ndauka’s Family ambapo kuna wasanii 15 wakiwemo wanamuziki na waigizaji. Mei 31, mwaka huu tulibahatika kutoa filamu ambayo inaitwa ‘Angela’ na staa aliyekuwepo ndani ya filamu hiyo alikuwepo Bi Hindu peke yake lakini waliobakia walikuwa ni underground waliokuwa chini ya Ndauka’s Family,” alifafanua Ndauka.
Kwa upande wake msanii huyo mpya wa Ndauka Music, [Casso] ameishukuru lebo yake hiyo kwa kumsaini pamoja na kuwaahidi mashabiki kuachia kazi nzuri.
Naye Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Aneth Mosha ameitaja sababu ya msanii huyo kuwa wa kwanza kutangazwa kwenye lebo yao hiyo ni kutokana na nidhamu aliyokuwa nayo, jitihada zake pamoja na kujituma.
img_2196
Casso akiongea na waandishi wa habari
img_2189
img_2187

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi