,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 21, 2016

Imekwisha timia jumla ya mikoa 14 ambayo team nzima ya Fiesta imekwisha weka kambi na kuhakikisha inadondosha mvua ya burudani katika kila mkoa kati ya hiyo 14.
Kila msanii ambaye alibahatika kupiga show katika jukwaa la Fiesta alionyesha ubunifu wake na ni jinsi gani anaweza kuwapaga wisha mashabiki pindi awapo jukwaani. Lakini kati ya wasanii ambao walionyesha utofauti mkubwa sana katika shows zao ni pamoja na msanii Benpol.
Kwasababu ni msanii ambaye ilikuwa ni vigumu kuitabiri show yake katika kila jukwaa kwasababu ya utofauti wa shows zake katika kila mkoa ambao alikuwa akitembelea kupiga show.
Phaijaona vibaya kumtafuta Benpol na kupiga nae story kutaka kujua ni kitu gani kajifunza au kajiongeza katika tour nzima ya mikoa 10 ya Fiesta ambayo alitembelea.

“Fiesta 2016 ilikuwa nzuri sana, me naweza kusema kama imenikuza hivi! Kwasababu imekuja kama changamoto kwangu, imenishughulisha sana, kwa maana nilikuwa najaribu kuonyesha vitu vya tofauti kwenye shows zangu. Kama umefuatilia shows zangu nyingi zilikuwa zina kitu tofauti ndani kias kwamba huwezi kufananisha. Shows zote 10 ambazo nimefanya Fiesta zote ni tofauti. Hata kama nyimbo zilikuwa zinajirudia lakini mpangilio wa show, vionjo vilivyomo ndani ilikuwa tofauti.”

Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo Benpol ameyazungumza, ngoja nikupe nafasi ya kumsikiliza yeye mwenyewe akifunguka juu ya hilo hapa chini kwenye hii video.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi