,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, October 20, 2016
TAARIFA KWA UMMA..........................

Wizara ya Mikopo chuo kikuu Dar es salaam inapenda kutoa mrejesho kama tulivyoahidi kurudisha mrejesho kwenu baada ya kuwafikia ama kuwasiliana na mamlaka za juu zaidi yaani Wizara ya Elimu juu ya hatma ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na Wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa ujumla


1: WANAFUNZI WANAOENDLEA NA MASOMO (CONTINOUS STUDENTS)
 

-Juu ya hoja zetu ambazo tulikuwa nazo dhidi ya Wanafunzi wanaoendelea na masomo (continuos students) kufanyiwa MEANS TESTED kama ambavyo tuliwaambia kwamba tunalipinga suala hili vikali ndiyo maana tukachukua hatua kufika ofisi ya makamu mkuu wa chuo (VC) ili sisi kama Viongozi tuweze kufika Ofisi ya Waziri wa Elimu kuelezea masikitiko yetu,Mawasiliano yalifanyika na Wizara ya Elimu na taarifa tulizozipokea palepale kwamba MEANS TESTED kwa wanafunzi wanaendelea na masomo kuwa Wizara imesikia hoja zetu na KUSITISHA MGAWANYO WA FEDHA KWA WANAFUNZI WANAOENDELEA (MEANS TESTED) na Majina ya Wanafunzi hawa tunatarajia kuyapata leo hii na tutayabandika leo hii katika mbao za matangazo maeneo ya CAFTERIA Mwaka wa masomo mnaoendelea tunashukuru kwa uvumivu wenu kwani sisi kama Viongozi tulikuwa tunatafuta taarifa muhimu zenye uhakika kwa mamlaka husika na siyo za kusikia.

2: MWAKA WA KWANZA
-Mpaka sasa tumepokea banchi ya kwanza ya mwaka wa kwanza majina 949 tofauti na matarajio yetu kwani ndaki za COHU,COSS,SOED na UDBS majina yao hayapo yakisubiliwa kutoka banchi ya pili
 

-Masikitiko yetu hata majina yaliyokuja hapa chuo kwa uchache wake yamefanyiwa MEANS TESTED hadi katika hela ya chakula na malazi mfano kuna mwanafunzi katika Vitabu (BS) amewekewa 7322/= wakati fedha ya kujikimu na chakula kawekewa sh.19216 kwa miezi miwili (siku 60) tofauti na Muongozo wa Bodi ya Mikopo unavyoelezea sehemu ya 3.1,3.3, hadi 3.4 "MEANS TESTED SHALL BE APPLICABLE TO FIRST TIME APPLICANTS ON TUTION FEES,SPECIAL FACULTY REQUIREMENTS LOAN ITEMS ONLY" hivyo basi Wizara ya Mikopo imeomba nafasi ya kuonana na Waziri wa Elimu yeye mwenyewe kuonesha masikitiko yetu kutokukubaliana na Mfumo wa mgawanyo wa fedha za Kujikimu kwa mwaka wa kwanza (MEANS TESTED) hoja zimeshaandaliwa kwa kuzingatia Muongozo wa Bodi ya Mikopo kama unavyoelezea hakutakuwa na mgawanyo katika fedha za malazi na chakula sh.8500/= kila siku na kwa vitabu sh.200,000/= {malipo ya mwaka wa masomo 2016/2017 }

Hivyo basi maadhimiyo yetu kama Viongozi ni kukutana na Waziri wa Elimu haraka kuonesha na kupinga mfumo huu wa mgawanyo wa fedha ya malazi na chakula kwa mwaka wa masomo 2016/2017
Zoezi la usainishaji wa fedha hizo linaanza rasmi siku kesho alhamisi tarehe kuanzia saa 3:00 asubuh mpaka saa 9:00 mchana
KARATASI ZA MALIPO YA MAFUNZO KWA VITENDO PIA ZITASAINIWA SIKU HIYO KWA WANAOENDLEA NA MASOMO
imetolewa na wizara ya Mikopo kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano mambo ya nje na Jumuiya za Wanafunzi
Kasunzu Eliud
0658202828
Mahmud Abdul
0659366125
Makupa Erick
0655191254

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi