,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, November 25, 2016

diamond-ommyUgomvi wa kurushiana maneno kati ya Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz umeendelea kushamiri kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wa pande zote mbili nao wakitoa maoni yao kuhusu wasanii hao. Leo Ommy Dimpoz amefanya mahojiano na Clouds Fm na kuzungumzia mambo mengi sana kuhusu uhusiano wake na Diamond tangu kabla hawajatoka na mikasa mbalimbali iliyowakumbua hadi kufikia leo hawazungumzi tena.
Baada ya Ommy Dimpoz kumaliza mahojiano hayo leo, Diamond ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagrama maneno haya;
“Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue😢😭
Tetesi zilizozagaa mitaani zinadai kuwa Ommy Dimponz amegombana na Meneja wake Mubenga baada ya kubaini kuwa meneja huyo ana uhusiano wa kimapenzi na na mpenzi wake (Ommy Dimpoz). Kufuatia tetesi, Diamond anadaiwa kurusha dongo hili kwa Ommy Dimpoz, “Sema kugombana na Manager wako kisa eti ana demu unaskia wivu hii ni #KOKORO zaidi!😭.”
Kwa upande mwingine, Wema Sepetu ambaye naye alitajwa kuwa ndiyo chanzo cha ugomvi wa wawili hawa kushamiri, naye hakubaki nyuma. Kuhusu mahojiano ya Ommy Dimpoz leo, Wema Sepetu aliandika, “Busara, Upole, Hekma… Thats wat u r made of… Im very very Proud and Impressed kwakweli… Mnyonge mnyongeni haki yaki mpeni… Sasa sio mje muanze kusema sijui napick sides… Nooooo…!!! Sina side maana na mimi pia ni outsider tu… But kwa leo nimependa ulichofanya Ommy…. Forever Bae… 👌🏽Sometimes being the bigger person doesnt hurt…”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi