kiba
Mwanamuziki Alikiba amechafua hali ya hewa baada ya kuposti picha yake wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa leo katika Mbuga ya Hifadhi ya Serengeti
na kuandika maneno kuwa anawaangalia Simba Original ambapo ujumbe huo umetafsiriwa kama kijembe kwa staa mwenzake Diamond Platnumz ambaye naye ujiita Simba.kingkiba
Kiba alitupia maneno hayo katika picha aliyoiweka kwenye akaunti yake ya Instagram ikimuonesha akiwa na darubini akiangalia kwa mbali simba waliokuwa juu ya mawe huku pembeni yake akiwa na mtu anayeonekana kuwa mwenyeji wa eneo hilo aliyekuwa anaendesha gari.
Picha hiyo imezua sintofahamu kwa mashabiki wa timu Kiba na Diamond ambapo walianza kutupiana maneno.
kiba

Baadhi ya comment za mashabiki hao ziko hapa;
#Unawapend simba ad umeenda kuwaona ha ha lazima utokwe pov chibu sio wa sport sport hapumulii mtu

#sie huku tunamuona Simba wa kuchora

#Hao kweli original datc why huwasogelei,,, wanaangalizka kwa darubin tyuuu hawa wengine huku mjin ni simba makaratac ndo maana wanakuogopa ww mr.Tanapa,,,, bday le king

#Dooooohhhh mmmmmhhh ebu ngoja nizime data nikuacheee yamekua hayoo tena

Baada ya picha hiyo Kiba aliendelea kuposti picha mbalimbali za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku nyingine akiwa na mwanamuziki mwenzake Baraka Da Prince.