,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, November 6, 2016

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imewapa siku 30 kuanzia Novemba 14, mwaka huu wadaiwa wake sugu 154,000 kurejesha fedha wanazodaiwa.
Vinginevyo, imesema watakamatwa na kulazimishwa kulipa madeni na gharama za kuwasaka.
Kwa mujibu wa bodi hiyo, wadaiwa wote wanaoangukia katika mkumbo huo, watatangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari Novemba 13, siku moja kabla ya kuanza kwa notisi hiyo ya siku 30, isipokuwa kwa wale ambao watakuwa tayari wamelipa.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul Razaq Badru alisema wadaiwa hao ni wa kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa ambao madeni yao yameiva.

Alisema hadi sasa serikali inadai Sh trilioni 2.6 kutoka kwa wadaiwa hao ambao walikopeshwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu lakini hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kuleta changamoto kwa waombaji wapya.

“Bodi itatangaza majina ya wadaiwa sugu wa kuanzia mwaka huo ambao madeni yao yameiva, majina yao tutayaweka hadharani Novemba 13, mwaka huu baada ya hapo tutawapa siku 30 kulipa, baada ya muda huo, hatua za kisheria zitachukuliwa na wahusika watalipia gharama za kuwasaka,” alisema Badru.

Alisema wadaiwa hao sugu wanapaswa kukumbuka kuwa kutolipa madeni yao ni kuvunja Mkataba na Sheria ya Bodi hiyo Namba 9 ya mwaka 2004, 19 (1).

Sheria hiyo ya mwaka 2004 Kipengele cha pili kinasema mdaiwa atapewa penalti ya asilimia tano juu ya ile asilimia tano iliyokuwa ikitozwa kabla, kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo. Aidha, kipengele cha tatu kinasema mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni lililoingiwa na bodi.

Vipengele vingine kwenye sheria hiyo vinasema mdaiwa atawekwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.

Pia mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa serikali au udahili wa masomo ya juu kwenye vyuo vyovyote ndani na nje ya nchi. Kadhalika, maelezo yao yatapelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi.

Badru alisema awali selikali ilitoa mikopo hiyo kwa wanafunzi, kwa kuweka bayana kwamba fedha walizopewa ni mikopo na wala si msaada au ruzuku, hivyo zinapaswa kujereshwa mara baada ya mdaiwa kuhitimu masomo yake; au pindi atakapositisha masomo yake kwa sababu mbalimbali.

Kuanzia mwaka wa masomo wa 1994/95 mpaka 2004/05, mikopo ilitolewa kwa wanafunzi kwa ajili ya kugharimia chakula na malazi pekee. Lakini kuanzia mwaka 2005/06 mpaka sasa, pamoja na gharama ya chakula na malazi, wanafunzi wanakopeshwa pia fedha kwa ajili ya kugharimia ada ya mafunzo, vitabu , viandikwa, mafunzo kwa vitendo, mahitaji maalumu ya vitivo na gharama za utafiti.

Akizungumzia ulipwaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo, Badru alisema jana (juzi) walisambaza katika vyuo vyote nchini zaidi ya Sh bilioni 71 kwa wanafunzi hao.

Usambazaji huo umefanyika baada ya vyuo vya elimu ya juu 13, kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wake, kama walivyoamriwa na wizara husika na kwamba vyuo viwili pekee, ndivyo bado havijawasilisha matokeo.

Pamoja na vyuo hivyo kutowasilisha matokeo hayo, bodi imewapelekea wanafunzi hao fedha na kwamba bodi itashughulika na vyuo husika kiutawala ili kuepusha wanafunzi hao kushindwa kuendelea na masomo.

“Wote tumewawekea fedha katika akaunti za vyuo jana usiku (juzi) kwa utaratibu maalumu kuhakikisha wanafunzi wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali wanapata fedha zao,” alibainisha Badru.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Maimuna Tarishi alivipa siku 15 vyuo vilivyokuwa havijawasilisha matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo, kuwasilisha ifikapo Novemba 2, mwaka huu.

Vyuo hivyo vilivyokuwa viwasilishe matokeo hayo siku 30 kabla ya kufunguliwa na kwamba utaratibu ni lazima vyuo kuwasilisha matokeo kuonesha wanafunzi wangapi wana sifa za kuendelea kupewa mikopo.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi