,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, November 6, 2016


DAR ES SALAAM: Dawa aina ya Thalidomide ambayo kama ikitumiwa na mama mjamzito husababisha mtoto kuzaliwa bila miguu na mikono, ugonjwa ambao kitalaam huitwa Phocomelia, inauzwa katika maduka ya dawa baridi jijini Dar es Salaam kama njungu, Risasi Mchanganyiko limegundua.
PHOCO-(3)Dawa hiyo ambayo jina lake jingine ni Synovir ilipigwa marufuku kutumiwa na wajawazito mwaka 1962  baada ya kuwafanya watoto zaidi ya 10,000 barani Ulaya kuzaliwa bila mikono na miguu, hutumika kutibu ugonjwa wa kujisikia vibaya wakati wa asubuhi kwa mama mjamzito mwenye mimba changa, hali ambayo kitalaam huitwa morning sickness.
PHOCOnn-(1)Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwenye maduka mbalimbali ya dawa jijini Dar umebaini kwamba, dawa hiyo inauzwa kwa watu hata wasio na cheti cha daktari kwa shilingi 1,800 kwa kidonge kimoja, jambo ambalo linahatarisha maisha ya watoto walioko tumboni kama atakayetumia ni mama mjamzito.


PHOCOb-(2)PHOCOMELIA NI UGONJWA GANI?
Phocomelia ni ugonjwa ambao chembechembe za mifupa ya mikono na miguu huathirika mtoto akiwa tumboni hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na kushindwa kukua vizuri na kufanya mtoto azaliwe bila mikono na miguu.
120901012909-thalidomide-5-horizontal-large-gallery
Ugonjwa huu ulianza kuonekana kwa mara ya kwanza duniani mwaka 1836 baada ya mwanasayansi wa Kifaransa, Etienne Geoffroy kuugundua na kuupa jina la Phocomelia, neno linalomaanisha ukosefu wa mikono na miguu.
Asilimia arobaini ya watoto ambao huzaliwa na ugonjwa huo hupoteza maisha kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja na ambao hufanikiwa kuendelea baada ya hapo, hulazimika kuishi maisha ya taabu kwa kutunzwa na watu wengine au kutumia sehemu ndogo ya viungo hivyo kuendesha maisha yao, ingawa hupata matatizo makubwa ya maumivu ya misuli wakitimiza umri wa miaka hamsini.
article-2649435-02A1362D0000044D-594_634x425Dawa za Thalidomide

Kufuatia watoto wengi kuzaliwa bila mikono na miguu, utafiti ulifanyika na kugundulika baadaye kuwa akina mama wajawazito waliotumia dawa ya Thalidomide kutibu ugonjwa wa kujisikia vibaya na kutapika wakati wa asubuhi ndiyo waliozaa watoto wenye tatizo hilo.
Pamoja na tatizo hilo kugundulika, Thalidomide iliendelea kutumika duniani mpaka ilipopigwa marufuku mwaka 1962, ikiwa tayari imekwishaathiri maisha ya watoto zaidi ya 10,000 katika nchi za Ulaya.

PA-14974335Dawa hiyo pia hutumika kutibu magonjwa ya ukoma na saratani ya damu iitwayo Multiple Myeloma.
Akizungumza na gazeti hili juu ya dawa hizo kuuzwa kama njugu, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nchini, Gaudensia Simwanza alisema kuwa dawa hizo zinapaswa kuuzwa kwa kibali maalum cha daktari tofauti na hivyo ni kosa kisheria.

DSC00858Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nchini, Gaudensia Simwanza.
Alisema kuwa dawa hiyo ilisajiliwa hapa nchini mwaka 2014, kuhusu kwa nini inauzwa kiholela, wafuatiliaji ni Baraza la Famasia ambao walichukua jukumu hilo mwaka 2011 baada ya baadhi ya sheria kubadilishwa na kupewa wao jukumu hilo.
Kwa upande wao, Baraza la Famasia walipotakiwa kufafanua suala hilo, walisema watafutwe Jumatatu (juzi) lakini ukweli ni kwamba wanafuatilia na dawa kama hizo zinazouzwa kiholela huwa wanazikamata na wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.
1.Naibu Waiziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee na Watoto,Dk.Hamis Kigwangala akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani).Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla hakuweza kupatikana kwani simu yake kila ilipopigwa iliita bila kupokelewa kama ilivyokuwa kwa waziri wake, Ummy Mwalimu.


NENO LA MHARIRI
Gazeti hili linalaani vikali uuzwaji holela wa dawa hizi kwenye maduka ya dawa na wakati mwingine kwa akina mama wajawazito bila cheti cha daktari, kufanya hivyo ni kuendelea kuathiri kizazi kijacho cha taifa hili ambacho ndiyo nguvu kazi inayotegemewa kusogeza mbele maendeleo.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi