,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, November 3, 2016

Kijana mweusi Danney Williams anayedai kuwa mwanawe rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ameomba kufanyiwa vipimo vya DNA.Williams aliwasilisha ombi hilo wakati mkutano aliofanya na vyombo vya habari katika mji wa Washington na kudai kwamba mgombea urais wa chama cha Democrats Hillary Clinton ni mamake wa kambo.Katika maelezo yake, Williams alisema, ''Mimi ni mtoto wa Bill Clinton. Hillary Clinton ni mamangu wa kambo na Chelsea ni ndugu yangu.''
Kijana huyo anayeishi katika jimbo la Arkansas alitoa ombi la kufanyiwa vipimo vya DNA ili kuthibitisha madai yake. Williams aliongezea kusema kwamba amekuwa akihangaika kufuatilia suala hilo tangu mwaka 1990 ili kutafuta uthibitisho.
Akibainisha kumpoteza mamake mzazi aliyeathirika kwa madawa ya kulevya tangu alipokuwa na umri mdogo, Williams aliitaka familia ya Clinton kuwasiliana naye.
Kwa upande mwengine, Williams alikanusha madai ya kusaidiwa na Donald Trump na kusisitiza kuwa alisimamia gharama za wakili mwenyewe huku akifahamisha kwamba madai yake hayana uhusiano wowote na uchaguzi mkuu ujao.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi