,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 22, 2016


Malisa GJ


Aliyekua Mbunge wa Kasulu Mjini Ndg.Mosses Machali ametangaza rasmi kujiondoa katika chama chake cha ACT Wazalendo na kujiunga na CCM. Katika sehemu ya taarifa yake kwa vyombo vya habari Machali amesema:


"Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli uatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono. Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona yakifanyika na sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono."

Machali anaongeza "Wale tuliopiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watendaji wanovu serikalini, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ya kuwachukulia hatua. Leo hii upinzani umepoteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri. Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Uongozi wa JPM unafanana sana na ule wa Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere...
....CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.
 

Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe.

Kwaherini Upinzani uliopoteza dira, nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo." MOsses Machali (X MP Kaasulu)

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi