,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 1, 2016

Mlimbwende mpya wa Tanzania mwaka huu 2016 amepatikana usiku wa Ijumaa katika Fainali ya Miss Tanzania iliyofanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza, huku siri ya ushindi wake ikivuja.
Kwa sasa siyo siri tena kuwa Diana Edward kutoka Kanda ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam ndiye Miss Tanzania mwaka 2016, baada ya kuwaangusha wenzake 29 waliopanda jukwaani katika Viwanja vya Rocky City Mall, jijini Mwanza.

Miongoni mwa siri kuu iliyomfanya Diana aibuke na ushindi huo ni uwezo wake wa kujieleza kwa kujiamini akiwa na hoja katika maelezo aliyotoa wakati akijibu swali alilochagua.

Siri nyingine ni kuchagua kusaidia jamii ya kabila la Wamasai ili waepukane na mila ya kukeketa watoto wa kike, akitumia msemo wa ‘Masai dondosha wembe’.

“Nia yake ya kutetea wasichana wa jamii ya Kimasai bila shaka ndiyo iliyowavuta majaji na kuamua kumtaja kuwa mshindi. Lakini namna anavyojieleza kwa kujiachia na kujiamini, ni kati ya sifa kuu zinazoangaliwa na majaji,” alieleza Julie Magesa, mmoja wa wahudhuriaji wa shindano hilo.

Magesa anaongeza “Amekuja na kitu cha tofauti.. angalia hata namna alivyozungumza, amechagua lugha ya Kiingereza, lakini amejibu vizuri, hana papara na ana pointi zinaoeleweka. Ni haki yake kuibuka mshindi.”

Mbali na ushindi wa Diana, warembo waliomfuata walikuwa ni Merry Peter kutoka Kanda ya Mwanza aliyechukua nafasi ya pili akifuatiwa na Grace Malikita wa Kanda ya Ilala aliyetwaa namba tatu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi