,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, November 28, 2016

Akiwa chini ya uongozi mpya wa Mukii International, M-Rap ameachia kazi yake mpya iitwayo ‘It’s Not Too Late’ aliyo mshirikisha Mayunga. Wimbo umetayarishwa na Bob Manecky wa AM Records huku video ikiongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.

Rapa M-Rap anayetikisa kwenye uga wa Bongo Fleva na ngoma yake hiyo mpya, ame funguka sababu za kubadili mtindo wake wa kuchana katika ngoma hiyo na kusema kuwa amebadilika ili kufuata soko la muziki huo kwa sasa.
mraplion-20160925-0001
M-Rap

M-Rap ambaye amezoeleka kama rapa zaidi kwa kutengeneza ngoma za kuchana zaidi huku

akifananishwa na ma’rapa’ wengine wanao endana kiumri kama vile Young D na Young Killer, katika ngoma hii mpya ameamua kuchanganya ladha na kuweka mitindo ya kuimba, huku yeye mwenyewe akiwa na ‘flow’ tofauti
Akiwa ndani ya FNL, Rapa huyo amesema muziki wa hip hop kwa sasa umebadilika, na ili msanii atoke, ni lazima abadilike kwa kuchanganya ladha tofauti huku akimtolea mfano Dogo Janja ambaye naye ameamua kubadilika katika siku za karibuni.
Amesema anaamini ngoma hiyo itakubalika kwa mashabiki na kwamba hawezi kupoteza mashabiki kwa sasa bali mashabiki wake wataongezeka kwa kuwa anawapa kitu wanacho kipenda.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi