,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, November 2, 2016

MAISHA MAGIC BONGO IKO JUU 
Multichoice Tanzania (DStv) inawaletea uzinduzi wa Maisha Magic Bongo utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 4 Novemba, kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Uzinduzi huu wa chaneli hii maalum kwa kazi za Kitanzania utaambatana na uzinduzi wa kazi mpya za wasanii kutoka Bongo zikiwemo Tamthilia na Filamu.Chaneli hii inazinduliwa rasmi tarehe 4 Novemba, 2016. Na baada ya hapo mtashushiwa manundo ya tamthilia za nguvu, zenye ladha ya kimapenzi na zinazotikisa mioyo yetu kama vile “Huba” na “Doli”. Bila kusahau kipindi kitamu cha “Harusi Yetu”, kipindi hichi kinalenga ziadi kwenye minuso ya kufunga ndoa na shamrashamra. Uzinduzi huu siyo mchezo, kwani utahudhuriwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Movies na watu maarufu nchini. Kwa kifupi, Multichoice Tanzania kupitia huduma yake ya DStv inayorusha chaneli ya Maisha Magic Bongo (160) imewaandaliwa mambo mazito na ya uhakika ili kuburudisha wateja wetu na kujivunia utanzania wetu kupitia kazi nzito za maproduza na waigizaji wetu wa Kitanzania.
Tumepata fursa nyingine ya kujivunia kama watanzania kupitia uzinduzi wa chaneli yetu ya kitanzania ya Maisha Magic Bongo (DStv 160) ambapo shughuli hii maalum itahusisha wageni kutoka sekta mbali mbali ikiwemo Filamu, Muziki, na wengine kibao ambao wamepata kadi zao za mwaliko.
Swali ni, Je umealikwa? 

“Are you invited?”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi