,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 1, 2016

Mali za Kampuni ya Mohamed Trans Limited yakiwemo mabasi yake vitapigwa mnada na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufidia kodi wanayodaiwa.
Mnada huo wa hadhara utaendeshwa na kampuni ya udalali iitwayo Sukah Security Company Limited & Court Broker waliopewa idhini ya kufanya hivyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Mnada huo utafanyika mkoani Shinyanga siku ya Ijumaa, Novemba 4, 2016 kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Yard ya Mohamed Trans Limited.Masharti ya mnada huo ni pamoja na mnunuzi kutakiwa kulipa asilimia 25 ya mali zitakazopigwa mnada papo hapo huku asilimia 75 zilizobaki zikilipwa ndani ya siku 14.
Kampuni hiyo pamoja na mali nyingine ilizonazo pia inamiliki mabasi ya Mohamed Trans yanayofanya safari zake kwenye mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Kagera, Dar es Salaam, Singida, Dodoma, Morogoro na Shinyanga.
Ukaguzi wa mali hizo unatarajia kufanyika kesho Novemba 2, 2016 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi