,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, November 2, 2016white_house_washington

Marekani ni moja ya mataifa makubwa duniani, ilipata uhuru wake Julai 4, 1776 kutoka kwa Uingereza. Hadi sasa Marekani imekuwa na Marais 44 ambapo Rais wa sasa wa Taifa hilo, Barack Hussein Obama ndiye Rais wa 44.

Likiwa ni moja ya mataifa tajiri zaidi duniani, utajiri wa wakuu wa nchi (Marais) waliioliongoza taifa hilo inatofautiana. Hapa chini ni orodha ya Marais 10 wa Marekani ambao wanautajiri zaidi.
10. Bill Clinton

Japo alikuwa ni mwanasheria mwenye mafanikio kabla ya kuingia kwenye siasa, utajiri wake mkubwa aliupata baada ya kutoka madarakani. Bill Clinton ni Rais wa 42 wa Marekani na  amekuwa madarakani tangu mwaka 1993 hadi 2001.
Kitabu chake kinachofahamika kama “My Life” kimeuza nakala zaidi ya milioni 2.2. Utajiri wake ni dola za Kimarekani milioni 55.
9. Franklin D. Roosevelt

FDR ni Rais wa 32 wa Marekani, ndiye rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote katika historia ya Marekani. Amekaa madarakani tangu mwaka 1933 hadi 1945 (miaka 12 na mwezi mmoja). Utajiri wake mwingi aliurithi kutoka kwa familia yake na alipomuoa mke wake Eleanor Roosevelt.
Utajiri wake ni dola za Kimarekani milioni 60.
8. Herbert Hoover

Hoover ni Rais wa 31 wa Marekani. Amekaa madarakani tangu mwaka 1929 hadi 1933. Tofauti na marais wengine ambao wengi utajiri wao waliurithi, Hoover yeye alikuwa ni yatima na ameweza kujitengenezea fedha kupitia biashara ya madini.
Utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 75.
7. Lyndon B. Johnson

Kufuati kifo cha JFK, Johnson alichukua ofisi katika moja ya vipindi vigumu nchini Marekani. Johnson ni Rais wa 36 wa Marekani ambapo alikuwa madarakani tangu 1963 hadi 1969. Utajiri wake mkubwa umetokana na mashamba makubwa anayoyamilikia katika jimbo la Texas.
Utajiri wake ni dola milioni 98 za kimarekani.
6. James Madison

James ni Rais wa 4 wa Marekani, anafahamiaka kama “Father of the Constitution.” Amekuwa Rais kuanzia mwaka 1809 hadi 1817. Licha ya kuwa alijipatia utajiri wakati akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali (secretary of state) na Rais, lakini utajiri wake zaidi aliupata kupitia mashamba zaidi ya ekari 4000 aliyonayo katika jimbo la Virginia.
Utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 101.
5. Andrew Jackson

Andrew ni Rais wa saba wa Marekani akiwa amekaa madarakani tangu mwaka 1829 hadi 1837. Utajiri wake mkubwa ameupata kupitia taaluma yake ya Kijeshi lakini pia mashamba makubwa anayoyamilikia.
Utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 119.
4. Theodore Roosevelt

Theodore alikuwa Rais wa 26 wa Marekani ambapo alikaa madarakani tangu mwaka 1901 hadi 1909. Japokuwa familia yao ilikuwa ni ya kitajiri wakiishi New York, Theodore alijitafutia fedha zake mwenyewe ambapo aliweza kujitengenezea utajiri kupitia uandishi wa vitabu. Kwa muda wake wote ameandika vitabu za 40 lakini pia mashamba makubwa.
Utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 125.
3. George Washington

Washington ni Rais wa kwanza wa Marekani, alianza kuongozi kuanzia mwaka 1789 hadi 1797. Utajiri wake mkubwa umetokana na umiliki wa mashamba makubwa. Katika jimbo la Virginia, kuna mshamba zaidi ya ekari 8000 alizokuwa akizimiliki.
Utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 525.
1. John F. Kennedy
President John F. Kennedy
Baba yake JFK alijitengenezea utajiri kupitia biashara mbalimbali alizozifanya kama vile biashara, kuuza vilevi, kutengeneza filamu na nyingine. JFK kiuhalisia hakuwa bilionea kwa sababu aliuawa kabla ya kurithi mali za familia, lakini wakati akiwa Rais, aliweza kuuongoza baadhi ya mashamba na biashara nyingine.
JFK alikuwa Rais wa 36 wa Marekani akiwa ameakaa madarakani kuanzia mwaka 1961 hadi 1963. Utajiri wake ni dola za kimarekani bilioni 1.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi