,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, November 20, 2016

MBUNGE WA ARUSHA MJINI AKIRUDISHWA LUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA 

Na Sosy

MCHUNGAJI Kiongozi wa kanisani la ELIMU PENTEKOSTE lililopo Longdong mkoani Arusha mchungaji, Simon Mollel, amehubiri na kunukuu maandiko ya biblia takatifu katika kile kinachodaiwa kumlenga mbunge wa jimbo la Arusha mjini Bwana Godbless lema, mchungaji Simon alinukuu andiko kutoka kitabu cha Warumi 13:1-3.

"Kila mtu aitii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasie mwenye mamlaka hushindwa na agizo la Mungu nao washindanao watajipatia Hukumu kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema Bali kwa sababu ya matendo mabaya,Basi wataka usimuogope mwenye mamlaka?fanya mema,nawe utapata sifa kwake".

Mchungaji alisisitiza kwa kukemea andiko la matusi lililoelekezwa kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha mhe Gambo mchungaji Simon alisema " andiko hili lilitumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu, kutoka Kwa simu ya mke wa mwanasiasa maarufu mkoani hapa, matusi ni chukizo mbele ya Mungu, achilia mbali kutukana mamlaka aliyoiweka na Mungu, baba kumtukana mtoto ni chukizo mbele ya Mungu, vile vile mtoto kumtukana baba ni chukizo mbele za mungu."

Mchungaji aliendelea kusema "Ujumbe uliotumwa kwa mkuu wa mkoa ni ujumbe mzito wa matusi ,ambayo hakika sidhubutu kutamka madhabahuni,ujumbe wa namna ile dhidi ya kiongozi mkuu ni kumkosea Mungu,mtuhumiwa anapaswa kutubu lasivyo Mungu ataendelea kumuadhibu kwa matendo yake makuu"

Mchungaji aliendelea kusoma maandiko matakatifu kutoka katika kitabu cha MITHALI 8:16 "KWA msaada wangu wakuu hutawala na waungwana,naam,waamuzi wote wa dunia" mchungaji Simon anaendelea kuhubiri "mamlaka zote chini ya jua zinabaraka na nguvu ya Mungu,yeyote ajionaye ananguvu kuliko mamlaka yaliyopo huwa chukizo mbele ya Mungu,Rais Magufuli aendeshavyo nnchi kuna nguvu ya Mungu ndani yake,matusi na kejeli dhidi ya Rais ni kumkejeli Mungu,huenda mh Rais hakuridhishi na utendaji wake,Hukumu pekee ni sanduku la kura sio kutoa lugha chafu na kutabiri mabaya dhidi ya Rais,kufanya hivyo ni chukizo mbele ya Mungu"

"Yuko mwanasiasa alisema Rais anajifanya yeye ni Mungu, naomba leo nimjibu, Rais hajifanyi yeye ni Mungu bali Rais Ana Mungu ndani yake, kumdharau ni makosa na machukizo mbele za Mungu. yeyote adharauye mamlaka humdharau Mungu."

Mchungaji alimaliza kwa kuwasihi waumini waendelea kuombea nchi na vilevile kuwaombea watawala, waitawale nchi katika mapenz yampendezayo Mungu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi