,./.,

\\..\\

W

=====

,,

... ...

...      ...

';';';';

';';';';
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 8, 2016Na Sosy
MKUU wa Mkoa kijana kuliko wote mwenye ubunifu wa hali ya juu Paul Makonda ameweka mikakati ya kuligeuza jiji hilo kuwa kama ulaya na muoenekana wa kisasa na kuwa mji wa kuvutia zaidi.

Moja yamipango yake ni kulifanya jiji hili kuwa safi ,kutenga maeneo ya biashara, usalama wa raia na mali zao, watumishi hewa, kurudisha hadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa, elimu na miundombinu bora, BLOG YA WANANCHI imeweza kuripoti.
Usafi; Makonda alitangaza zawadi ya gari la Sh20 milioni au fedha taslimu kwa mwenyekiti ambaye mtaa wake utaongoza kwa usafi na Sh5 milioni kwa kila mjumbe wa mtaa husika. Zawadi hiyo itakayokuwa ikitolewa kila baada ya miezi mitatu, itaanza rasmi Aprili Mosi
Ni kiongozi mwenye falsafa ya kipekee katika uongozi ya kuamini maendeleo katika uchapakazi na kwamba yeye hapendi nyakati za kufanya kazi kufanya siasa.
“Ninyi ni kama viongozi wengine, nataka mtimize ahadi zenu mlizowaahidi wananchi kipindi cha kampeni siyo kuleta siasa. Tushirikiane kuleta maendeleo katika jiji hili linalotazamwa na kila mtu” hii nin kauli yake alipokuwa akizungumza na watendaji 559 wa mkao huo.
Maeneo maalumu ya biashara; Kiongozi huyu mbunifu anataka mji wa Dar es Salaam kuuweka katika mazingira mazuri haswaa kwa kutenga maeneo mazuri ya biashara ambapo wafanaya biashara watakuwa katika mazingira rafiki kwa biashara zao pamoja na kuweka utaratibu nzuri wa kukusanya mapato.
Ninatamani kuona Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temeke zikitenga maeneo maalumu kwa ajili ya maduka ya magari na gereji pia.
Usalama; Makonda amekuwa makini katika suala la usalama watu na mali zao kwa juhudi kubwa za kujenga vituo vya Polisi vikubwa 20 katika jiji la Dar es Salaam ambalo awali lilikuwa lina matukio mengi ya ujambazi.
Ametoa Motisha  kwa jeshi ya kutoa zawadi ya shilingi milioni 1 kwa askari atakaye mtia nguvuni jambazi na waharifu wengine.
Amekuwa akiumizwa roho akisikia matukio ya kikatilii yametokea ambapo tayari ameonekana akidhihirisha kuchukizwa kwa matendo hayo kama alivyoendesha harambee ya kumchangia kijana Saidi Mrisho aliyetolewa macho na Salum Nywete alimaarufu Scopioni.
Elimu, Makonda yeye ni kijana msomi anatambua umuhimu wa elimu na kwamba amekuwa mstari wa mbele kuchangia madawati na ujenzi wa shule mbalimbali Mkoani Da es Salaam,
Pia aliwahikuwataka watendaji na wenyeviti katika mitaa yao kutafuta wadau kusaidia sekta hiyo badala ya kusubiri Serikali.
 Miundombinu; tangu Makonda akabidhiwe Dar es Salaam  tayari kuna mabadiliko katika ubora na wingi wa miundombinu ikiwa pamoja na kupungua kwa foleni kero ya wananachi wa mji huu ya foleni barabarani.
Wananchi wa Dar es Salaam, wamebahatika kuongozwa na kiongozi kijana mwenye ubunifu wa hali ya juu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi