,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 29, 2016

14624632_579954458855754_2472429113994903552_n
Jux amefunguka kuhusu timu zilizopo kwenye muziki hapa nchini. Hivi karibuni timu hizo zimeonekana kuchafua hali ya hewa mitandaoni kwa kutukanana matusi mazito huku baadhi ya wasanii wakikumbana na mvua hizo za kashfa na matusi.

Hitmaker huyo wa Wivu, amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez kuwa timu zinasaidia wasanii kufanya vizuri ila hazitakiwi kufika mbali zaidi hadi kutaka kushikana mashati.
“Muziki wetu sometimes unakuwa unalala sana, unatakiwa uchangamke. Unajua kunapokuwa na timu hata msanii unayekuwa unashindana naye kazi zinakuwa zinafanyika kwa ubora mtu anakuwa hakuchukulii poa. Lakini kitu ambacho sikipendi kwenye hizo timu zisifikie hatua zikaanza kushikana mashati, kuchomana mavisu sijui nini,” amesema.
“Mimi mwenyewe na Ben Pol ni wapinzani wakubwa tu, lakini tukitoka kwenye stage au studio ni washkaji lakini kikazi akitoa video ananiambia kaka nimeshakunyoosha na mimi namuambia utaona,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi