,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 15, 2016

Balozi Mpya wa Multichoice Tanzania Msanii Joti Akizungumza na Waandishi wa Habari leo wakati wa Uzinduzi Mkubwa wa Punguzo la Bei ya Kifurushi kwajili ya Wateja wa DSTV leo. Multichoice Tanzania katika kusherehekea msimu huu wa Sikukuu, inawaletea zawadi  kubwa  wateja wake kwa kufanya mapinduzi makubwa kupitia punguzo la bei na kuongeza chaneli  nyingi zaidi kwenye kifurushi cha DStv Bomba. Mabadiliko haya yanaanza rasmi leo tarehe 15 Novemba, 2016. Habari hii ilitangazwa rasmi kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliyofanyika hoteli ya Serena tarehe 15 Novemba.

Kifurushi cha DStv Bomba kina mabadiliko, bei yake mpya kuanzia leo tarehe 15 Novemba ni sh. 19,950, bei ya zamani ilikuwa TZS 23 500.  Chaneli zaidi ya 5 zimeongezeka kwenye kifurushi hiki zikiwemo: B4U Movies, SuperSport 4 and Eva Plus, Supersport 12 na FoxLife. Wateja wataendelea kufaidi burudani za hali ya juu zikiwemo mechi zote za Laliga, michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON 2017), Mashindano ya Kimataifa ya Riadha yote kupitia Superspot 4, filamu na Tamthilia mpya kabisa kutoka Bongo Muvi ambazo hazijawahi kuonekana kabla zitaonekana sasa kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo,  Telenovelas kutoka Telemundo na chaneli mpya ya Eva Plus, Tamthilia za kihindi ndani ya Zee Wold ,  vichekesho, vipindi vya watoto, muziki na mengine kibao kwenye kifurushi hiki cha DStv Bomba.

Pamoja na hayo, Multichoice Tanzania imemtangaza rasmi balozi wake wa mwaka 2016/17 kuwa ni “Joti”, ambaye ni mchekeshaji maarufu nchini. Balozi huyu atasaidia kuiwakilisha na kuitangaza Multichoice Tanzania, huku akivuta mkazo kwenye huduma bora zinazotolewa na kampuni hii katika kuburudisha wateja wake.

Nia yetu katika kufanikisha punguzo hilo la bei ni kuweza kunufaisha wateja wetu ili kuwapa huduma bora zaidi na kuthamini mchango wao katika muendelezo wa kampuni yetu.  Multichoice tunayo furaha kubwa kuwaalika wateja wapya ili waweze kufaidi kupitia huduma zetu. Mapinduzi haya ya punguzo za bei ni mwamko mkubwa sana katika kufanikisha malengo yetu sio tu hapa nchini, lakini Afrika nzima.

Kwa maelezo zaidi tufatilie: Instagram , Facebook (@dstvtanzania), (https://www.facebook.com/DStvTanzania/), https://www.dstv.com/.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi