,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, November 5, 2016

ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA MTAA KWA MTAA

JESHI Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke limeanza operesheni ya tokomeza ‘Panya road’ kwa kufanya msako wa mtaa kwa mtaa ili kukomesha makundi ya vijana wenye nia ovu ya kufanya uhalifu  pamoja na uporaji, wizi kutumia silaha, na makundi mengine ya kihuni.




Operesheni hiyo itawashirikisha wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji watakao ongozana na askari wa jeshi hilo kuwasaka vijana hao katika mitaa mbalimbali ya Temeke.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Giles Muroto akizungumza na Wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na watendaji wa wilaya ya Temeke amesema hali ya Usalama katika ukanda wa Temeke na Mbagala inatia shaka hasa kutokana na vijana wadogo chini ya Miaka 18 kujihusisha na Uhalifu.

Amesema wananchi wasioshiriki ulinzi shirikishi watachukuliwa hatua kali ikiwemo kutozwa faini ya Elfu hamsini pamoja na kifungo cha miezi sita jela, huku wenyeviti wa mitaa wametakiwa kuwatambua wakazi wao kinyume chake watakuwa matatani pindi uhalifu utakapotokea katika mitaa yao.

Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Nasibu Mbaga amewataka wenyeviti hao kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kuhusu suala la ulinzi na Usalama ambapo pia Mkurugenzi wa TRA mkoa wa Temeke amewataka watendaji kuhakikisha wanatoa Ushirikiano katika Ukusanyaji wa kodi za majengo.


0 comments:

Post a Comment

ufunguzi