,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, November 3, 2016
Moja ya jengo la lenye vyumba vya madarasa 4, katika shule ya msingi Sima 'B' ambalo limejengwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokea (mpango kwa matokeao) (P4R) Program Four Result. ambapo kumejengwa vyumba vya madarasa 8 shuleni hapo.

Moja ya jengo la lenye vyumba vya madarasa 4, katika shule ya msingi Sima 'B' ambalo limejengwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokea (mpango kwa matokeao) (P4R) Program Four Result. ambapo kumejengwa vyumba vya madarasa 8 shuleni hapo.

Baadhi ya walimu shule ya msingi Sima 'B' halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, wakiwa katika hafla ya kukabidhi vyumba vya madarasa 8 vilivyojengwa shuleni hapo kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeao (P4R) Program Four Result.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkzedek Humbe akiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Sima 'B' iliyoko katika halmashauri hiyo mkoani Simiyu wakati wa hafla ya kamati hiyo kukabidhi vyumba vya madarasa 8 vilivyojengwa shuleni hapo kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeao (P4R) Program Four Result kwa mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkzedek Humbe akikagua madarasa hayo pamoja na madawati kabla ya kukabidhiwa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkzedek Humbe akikagua madarasa hayo pamoja na madawati kabla ya kukabidhiwa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkzedek Humbe akikagua madarasa hayo pamoja na madawati kabla ya kukabidhiwa.

Mwalimu Shule ya Msingi Sima 'B' Michael Gimbuya Akisoma taarifa za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa mbele ya Mkurugenzi wa halmashauri kabla ya kukabidhi.
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu inaweza kuwa halmashauri ya kwanza nchini kwa kumalisha ndani ya muda ujenzi wa vyumba nane katika shule zake mbili za msingi, Sima 'B' pamoja na Kidinda kupitia mradi wa lipa kutokana na matokeo (P4R) Program Four Result.

Akiongea katika makabidhiano ya majengo hayo kutoka kwenye kamati ya shule na Halmashauri ambayo yaliyofanyika jana katika shuleMkurugezi huyo alisema kuwa ni jambo la heri kwa kufanikisha usimamizi wa ujenzi huo kutokana na kutumia muda mfupi uliowekwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo na serikali wa siku 90.

Alisema kuwa serikali ilitoa kiasi cha milioni 192 kutoka wizara ya elimu huku ikiwapa muda wa siku 90 kukamilisha ujenzi huo vyumba vya madarasa nane pamoja na matundu ya vyoo 20 pamoja na kukarabati
majengo ya shule.

“serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa kwa lengo la kuangalia mfumo mpya wa kutokutumia wakandarasi katika ujenzi na tulipewa muda wa kutekeleza ndani ya siku 90 na tumefikia malengo “alisema Humbe.

Aliongeza kuwa chumba kimoja cha darasa kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 20 ikiwa na pamoja na umeme na madawati yake 15 tofauti na kuweka mkandarasi ambaye angeweza kutumia Zaidi ya fedha hizo.

Aliongeza kuwa halmashauri hiyo imetumia muda wa siku 65 badala ya 90 walizopewa na serikali kukamilisha majengo hayo, hali ambayo alisema inawezekana ikiwa halmashauri ya kwanza kutekeleza kazi hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Masunga Maligende alisema kuwa baada ya kupata mradi huo walikaa na kuangalia namna ya kutumia wakandarasi wanaozunguka shule hiyo ili kurahisisha gharama za ujenzi.

“tulipata mawazo sana kamati yangu ya shule baada ya fedha kuingizwa kwenye akauti tukiangalia na muda tuliopewa ili kukamilisha mradi huo wengi wetu wanakamati tulikuwa na wakati mgumu lakini kwa umakini wetu tumeweza kukamilisha ujenzi huo ndani ya wakati”alisema Maligende.MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi