,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, November 12, 2016


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amedai wimbo ‘Nakula Ujana’ ni wimbo ambao umemwingizia pesa nyingi kuliko nyimbo zake zote zilizopita.

Rapa huyo ambaye amejizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake za shari, amedai Nakula Ujana ni wimbo ambao ulipingwa na watu lakini bahati nzuri ukaja kufanya vizuri.

“Nakula ujana wakati natoa audio asilimia kubwa ya wadau walikua na wasiwasi kuwa hauwezi kuwa hit. Wachache ndio walikua upande wangu kwamba wimbo utakuwa hit na utakua gumzo akiwemo Marco Chali ambaye alishiliki ku produce hii Ngoma,” aliandika Nay wa Mitego Instagram. “But baada ya Kutoa Video wimbo Huu ukawa Gumzo kila sehemu Na ukaleta Misemo kibao (Slogan) na mpaka leo hii, #NakulaUjana ni moja kati nyimbo zilizo nifanya niingize mkwanja mrefu kuliko nyimbo zingine za nyuma. Nilipata show nyingi na matangazo pia,”

Rapa huyo kwa sasa yupo mkoani Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya show ambayo itafanyika weekend hii.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi