,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 8, 2016

Meneja na muanzilishi wa kundi la Yamoto Band, Said Fella amesema kundi hilo kukosa tuzo mbili kubwa mfululizo yeye anachukulia kama mafanikio.

Kwani kuchaguliwa tu kuingia kwenye kipengele cha tuzo kubwa kama za MTVMAMA’s na zile za Afrima ni ushindi tosha hivyo yeye anaona ni mafanikio tosha kwani hata hivyo wapo wasanii wakubwa ambao hawajawahi kupata Fursa kuchaguliwa hata mara moja kwenye tuzo za kimataifa.
yamoto_band_-20161108-0001
Yamoto Band
Said Fella ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilungule iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam aliongea hayo kwenye Kipindi cha Faceoff cha Dizzim.
Fella alisema kuwa, Wingi wa show pamoja na Maandalizi ya kurekodi vipindi vya Coke studio Africa ni moja ya vitu ambavyo vimefanya wakawie kutoa wimbo mpya lakini hata hivyo mashabiki wa Yamoto Band wategemee mazuri mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili kwani kuna wimbo umeshaandaliwa na utakuwa ni funga mwaka.
Said Fella mbali na kusimamia kundi hilo maarufu Afrika ya Mashariki pia ameanzisha kundi lingine la muziki wa Taarabu linaloitwa YA TMK MODERN TAARAB, lakini kama haitoshi pia nae anakamilisha list ya mameneja watatu wa msanii maarufu Barani Afrika Diamond Platnumz.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi