,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, November 12, 2016

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI HODHI YA  RASILIMALI ZA RELI (REHCO),MASANJA KADOSA


Na Sosy
BAADA ya Serikali  kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa reli ya Standard Geuge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza tayari inakamilisha  reli ya ndani ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza adha ya foleni.
KaimMkurugenzi Mtendanji wa kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania REHCO Masanja Kadosa amesema kuwa serikali imetenga Trilion 1 kwa ajili ya ujenzi huo.
amesema kuwa ujenzi wa reli za ndani utakamilika Mwezi Desema mwaka huu.

"Kuna Mradi wa kujenga reli mpya katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kwa ajili ya treni za abiria ili kupunguza msongamano wa abiria na magari. Mradi huu uko katika hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali chini ya kampuni ya ushauri ya GIBB Engineering ya Afrika Kusini na kwamba inatarajiwa kukamilika Disemba 2016,” alisema.


HATA hivyo  ujenzi wa reli ya Standard Gauge kutoka Jiji la Dar es Salaam kwa awamu ya kwanza  itaanza rasmi Disemba 6, 2016.

"Ujenzi wa reli ya standard gauge umeshaanza lakini hatua iliyokuwepo haionekani, tenda zimeshaanza kutangazwa,”alisema Kadogosa wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema ujenzi huo utaanza kwa awamu na kwamba awamu ya kwanza inatarajiwa kuanzwa Disemba 6, 2016 wakati ya pili itaanza Februari 15, 2016.

“Ujenzi huo utachukua miaka mitatu kukamlika, ambapo utaleta manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Pia utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutokana na kwamba litakuwa na mabehewa yenye kilomita 2 ambayo sawa na ukubwa wa malori 300,” alisema.

Alisema wamiliki wa majengo yatakayo athiriwa na ujenzi huo watalipwa fidia.
“Hifadhi ya reli ina maana kwamba kila upande inaachwa mita 30, hivyo kama kuna nyumba zitakazokuwa nje ya mita hizo zitatakiwa kubolewa wamiliki watalipwa fidia,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi