,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, November 30, 2016

Mandatory Credit: Photo by Andrew H. Walker/WWD/REX/Shutterstock (5585909l) Kanye West Yeezy show, Runway, Fall Winter 2016, New York Fashion Week, America - 11 Feb 2016
Kanye West ataendelea kubaki hospitali kwa muda usiojulikana.

Tovuti ya TMZ iliripoti kuwa Yeezy alikuwa aruhusiwe kutoka hospitali Jumatatu hii (Nov. 28). Vyanzo vilidai kuwa daktari wake angeendelea kumwangalia akiwa nyumbani. Hata hivyo, West ataendelea kukaa hospitali bila taarifa ya lini anaweza kuruhusiwa.
West amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili kwa muda sasa. Bado anaendelea kuangaliwa katika hospitali ya UCLA Medical Center huku akikataa hata kuguswa na madaktari kutoka na uoga.
Mke wake, Kim Kardashian yupo kwenye wakati mgumu kiasi cha kuweka kila kitu pembeni na kuwa na jambo moja tu – kumwangalia mumewe huyo aliyelazwa tangu wiki iliyopita.
458451494_kim-kardashian-kanye-west-zoom-1ba3f535-c4a1-49e1-b7ef-ecb49d47593a
Vyanzo vimeiambia tovuti ya TMZ kuwa Kim amekuwa kwenye wakati mgumu tangu avamiwe na majambazi mjini Paris, Ufaransa lakini tangu Kanye apate matatizo wiki iliyopita kila kitu kwake kimebadilika. Vyanzo hivyo vimesema kuwa Kim amekuwa kama mwokozi wa Kanye na amekuwa macho muda wote akimwangalia mume wake aliyelazwa kwenye hospitali ya UCLA Medical Center kwa wiki sasa.
Vyanzo vimesema amekuwa na mtihani kwake hasa kwakuwa kuna wakati Kanye amekuwa akizungumza kuwa watu walikuwa wanataka kuivunja ndoa yake. Ni moja ya chanzo cha mashaka yake makubwa.
Kim, anatarajiwa kumrudisha Kanye nyumbani Jumatatu hii na lengo lake ni kuhakikisha anarejea kwenye afya yake. Chanzo kimoja kimesema Kim amejitoa haswaa na kwamba Kanye ana bahati kuwa naye.
“She has been an unbelievably devoted spouse. He’s a lucky man.”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi