,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, November 28, 2016

Mkuu wa shule ya Academic International Tanzania Shyama Santhosh. 

Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti juzi na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa China, Inder Jit Sagar.

Dar es Salaam. Wanafunzi wawili wa Shule ya Academic International Tanzania, wameweka historia katika mitihani ya mtalaa wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya kwanza duniani kwenye masomo ya hisabati na kompyuta.
Harshvardhan Babla amekuwa wa kwanza mtihani wa somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa kidato cha tano, huku Abishek Sankaranarayanan akishika nafasi ya kwanza katika somo la Hisabati kidato cha nne.

Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti juzi na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa China, Inder Jit Sagar.
Pia, walimu wa masomo hayo; Thadei Mwinuka anayefundisha somo la Kompyuta na Walter Mlowe wa Hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi.

Akizungumza katika hafla maalumu ya kuwapongeza, mkuu wa shule hiyo, Shyama Santhosh alisema wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule, walimu na nchi.

“Huu ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu na nchi, mtihani wa Cambridge unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia hii inaonyesha walimu wetu wapo makini,” alisema.

Source:- Mwananchi Blog

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi