,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, November 12, 2016

NavykenzoMakala: Imelda Mtema
NAVY Kenzo ni mojawapo ya makundi yanayofanya vizuri hivi sasa katika sanaa ya Muziki wa Kizazi Kipya, likiwa linaundwa na wasanii wapenzi, Aika Mariale na Emannuel Mkono maarufu kama Nahreel, ambao wanatamba na kibao chao cha Kamatia Chini.Kwa pamoja wanamiliki studio yao, The Industry na juzikati walizungumza na Risasi Vibes.
Risasi Vibes: Mashabiki wangependa kujua safari yenu ilianzia wapi?
Navy Kenzo: Tulikutana

 India mwaka 2008, kila mmoja alikuwa shule kivyake, tulikutana katika ule mkutano wa wanafunzi Watanzania.
Risasi Vibes: Uhusiano ukaanzia hapo?
Navy Kenzo: Hapana, ila pale tulijuana vizuri ni wapi mtu anaweza kumpata mwenzake na mara nyingi tulikuwa tukitembeleana katika hosteli zetu tunazokaa. Tunapokutana ilikuwa lazima ukute mmoja anasikiliza nyimbo kwenye simu mwingine anaimba.
Kuna siku tukaambizana mbona kama wote tunaweza muziki, kwa sababu Nahreel alikuwa prodyuza toka shule na mimi Aika, naimba, tukapanga tukirejea nyumbani tufanye kitu.
Risasi Vibes: Kwani huko shule mlienda kusomea muziki?
Navy Kenzo: Hapana, kila mmoja alikuwa anasomea kitu chake, Nahreel alisomea Computer Science na mimi Bachelor of Business Admnistration.
Tulivyorudi mimi nikaenda kwetu Arusha, yeye akabaki Dar, nilienda kufanya kazi katika kampuni ya baba yangu, nikamshauri aje Arusha sababu kule wanamuziki wengi.
Risasi Vibes: Kwa hiyo ndiyo mkaanzia huko huko kutengeneza kundi lenu?
Navy Kenzo: Hapana kwa sababu baadaye mwenzangu alijiunga na Pah One, kwa hiyo hata mimi nilikuwa kama tu kukitokea kitu naimba nao.
Risasi: Ikawaje sasa mkaingia kwenye uhusiano rasmi na kukaa pamoja?
Navy Kenzo: Baadaye nilikuja Dar, nikaungana na Nahreel ambapo hapo sasa ndiyo tulipoanza msoto wetu.
Risasi Vibes: Kivipi?
Navy Kenzo: Nilipokuja Dar, tukaanza kutafuta nyumba kila tukigusa ni bei kubwa sana na sisi hela hiyo hatukuwa nayo, mwisho ikabidi tupate chumba maeneo ya Mikocheni.
Risasi Vibes: Hapo ndipo mlipokuwa na studio?
Navy Kenzo: Ndiyo, maana sebule ndiyo ilikuwa studio na huwezi amini, ndani tuna godoro, tena dogo sana, wakati mwingine tunajikuta tumelala sakafuni.
Risasi Vibes: Sasa hela zenu mlikuwa mnazipataje?
Navy Kenzo: Yaani we acha tu, kuna kipindi tulikosa hela kabisa hadi tukawa tunashinda na njaa, nakumbuka kulikuwa na duka la Mangi karibia na kwetu, tukawa tunakopa tukipata hela tunalipa.
Risasi Vibes: Kwa hiyo mlishawahi kushinda na njaa kabisa?
Navy Kenzo: Tena siyo mara moja, hapa mimi na yeye wote tunaumwa vidonda vya tumbo kwa sababu ya kushinda njaa.
Risasi Vibes: Lakini familia zenu zinajiweza, ilikuaje sasa?
Navy Kenzo: Ni kweli wote tumetokea katika familia nzuri, lakini kuna kitu tulijifunza kutoka kwa wazazi wetu kuwa lazima ujifunze kutafuta ili uweze kuishi vizuri na ndicho tunachofanya kwa sababu tulilelewa maisha mazuri na sisi tunataka watoto wetu pia waje kuishi vizuri.
Risasi Vibes: Kuna tetesi kuwa familia zenu hazikubariki uhusiano wenu ni kweli?
Navy Kenzo: Mara nyingi inatokeaga hivyo, lakini mwisho wa siku wanakubali wakiona msimamo wetu!
Risasi Vibes: Mlipataje studio kubwa mlipokuwa mkiishi?
Navy Kenzo: Yaani ni Mungu tu na juhudi zetu kwa sababu tulivyoanza kutoa nyimbo na kupendwa tuliweza kupata michongo mbalimbali ndiyo tukaweza sasa kutengeneza studio ya kisasa.
Risasi Vibes: Kuna tetesi kuwa mmenunua kiwanja hapo mlipopanga, je zina ukweli?
Navy Kenzo: Unajua kipindi tunapanga pale Mikocheni, pembeni yetu tukawa tunaona kiwanja kiko wazi tukawa hatuelewi cha nani lakini huwezi amini mimi na mwezangu tukasema ipo siku kitakuwa chetu na Mungu ni mwema siku tukakutana na mwenye kiwanja tukazungumza naye na tukaanza kukilipia kidogokidogo.
Risasi: Kwa hiyo mpaka sasa ni sehemu yenu wenyewe?
Navy Kenzo: Ndiyo, tunamshukuru Mungu kwa hilo.
Risasi: Kwa kuwa mmetoka mbali, vipi kuhusu mpango wa kufunga ndoa?
Navy Kenzo: Hiyo ipo tu wala haikwepeki, tunaweka mambo vizuri.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi