,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, November 21, 2016

Serikali imetakiwa kuangalia upya tozo za magari ya watumishi wa serikali wakati wa kuvuka daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (kwanza kulia) akieleza changamoto za wilaya hiyoMkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, ameyasema hayo leo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kuangalia na kutatua changamoto za wananchi wa eneo hilo.
Alilitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuangalia upya tozo hizo za magari ya Halmshauri hiyo na watumishi wa umma wanaoishi nje ya Halmshauri kutozwa fedha kuvuka katika daraja hilo jambo ambalo linaleta changamoto kubwa kwa na kuwaongezea sababu.
“Kila gari ya Halmashari inayopita katika daraja hili inatozwa fedha ya shilingi 2000,hasa ikizingatiwa kuwa halmashauri hii ni mpya hivyo watumishi wengi wanatokea nje ya halmashauri,”alisema.Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la tozo la daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara, alikiri kupokea malalamiko ya watu wengi kutaka kupunguziwa au kuondolewa tozo hiyo.“Ni kweli tumekuwa tukipokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi mbalimbali, lakini suala ni kwamba sisi kama NSSF huwa hatupangi viwango vya tozo za kuvuka daraja bali tunapokea maelekezo kutoka wizara husika (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi),”alisema.
Aliongeza kuwa atawasilisha suala hilo katika wizara husika ili kuona uwezekano wa kuondoa tozo hiyo ama kupunguza.Kahyarara alitaja changamoto zingine kuwa ni uwepo wa vijana kuligeuza daraja hiyo kuwa kijiwe na wengine kuwa na nia ovu ya kulihujumu kwa kuharibu miundombinu, ingawa ulinzi umeendelea kuimarishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kigamboni
Kwa upande wake RC Makonda amesema chanzo cha magari ya Halmashauri hiyo kutozwa tozo ni kutokana na mchakato na ujenzi wa daraja hilo kufanyika kabla ya Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni kuanzishwa.
Katika hatua nyingine DC Mgandilwa alimuomba RC Makonda kuangalia uwezekano wa kuunganisha barabara ya vumbi eneo la Vijibweni kutoka daraja la Nyerere lenye urefu wa kilometa 1.5 ili kuondoa adha ya wananchi wanaotumia barabara hiyo.
“Hii barabara licha ya kutumiwa na magari mengi yanayopita katika daraja hili, lakini haijajengwa kwa kiwango cha lami hivyo wananchi kupata kero kubwa kutokana na vumbi na magari kugonga mawe tunaomba utusaidie,”alisema Mgandilwa.
Akihutubia wananchi wanaoishi karibu na mradi wa daraja hilo,RC Makonda amewahikishia kuwa barabara hiyo itaanza kujengwa baada ya wiki mbili ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wananchi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi