,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, November 15, 2016

Ilikuwa Ijumaa ya November 11 (Ijumaa iliyopita) ambapo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm ngoma ya mwanadada Nandy ya “Nagusa Gusa” ilisimama kama jiwe la wiki ijumaa hiyo.
Kama ilivyo kawaida, Nandy alikuwepo mjengoni kupiga story mbili tatu kuhusu muziki wake na vitu kama hivyo. Moja kati ya maswali ambayo aliulizwa mwanadada Nandy ni pamoja na mafanikio gani ambayo ameyapata kupitia tour ya Fiesta, ni fursa gani ambazo amezitumia kwenye msimu huo.
Alichokijibu mwanadada Nandy ni “Kutengeneza connection nzuri na wasanii wenzake, kuandaa mazingira ya kufanya collabo na vitu kama hivyo.”

Ndipo Bdozen alipoamua kumuuliza ni collabo ngapi tuzitarajie kutokea kama mazao ya Fiesta, akiwa na maana kuwa ni wasanii gani amekwisha fanya nao mazungumzo na kukubaliana nao kufanya collabo, na hata wale ambao wamemuomba yeye pia.

Vanessa Mdee, Darassa, Mr Blue, Billnass pamoja na Raymond ni wasanii ambao Nandy aliwataja kuwa amekwisha waomba collabo na chochote kitarajiwe baina ya Nandy na wakali hao.

Nandy aliwataja Nikki wa Pili, Man Fongo pamoja na Shilole kama wasanii ambao wao ndio walimuomba collabo.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi