,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, December 1, 2016

Msanii na pia ni Meneja wa msanii mwenzake kutoka Kenya, Akothee. Jaguar ambae kwa sasa ameamua kujikita zaidi kwenye shughuli za kiserikali ili kusudi kuwasaidia wananchi wa Kenya.

Ni wiki sasa imepita baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa maji na Wizara ya Maji na Umwagiliaji Nchini Kenya, msanii Charles Njagua Maarufu kwa jina la Jaguar.
Jaguar amesema atafanya kampeni kuhakikisha kuwa wakazi wa vitongoji duni vyote nchini wanapata maji safi na Salama.
WhatsApp-Image-2016-11-30-at-00.20.19-295x300
Msanii Jaguar Akiwa na Wananchi huko Kibera nchini Kenya.
Msanii huyo ambaye pia ni mwanachama wa bodi ya halmashauri ya kupambana na matumizi ya mihadarati nchini Kenya, NACADA amesema kuwa uteuzi huo ni wa Heshima kwake na yeye atajitahidi kuonesha vitendo kwa kuwasaidia watu wasiojiweza na kunufaika na Taifa lao.
Huku akiahidi kufanya kazi kiuadilifu kama Rais Magufuli, Tanzania.
“Nimeaminiwa kufanya kazi na wakenya wote hivyo nitafanya kazi kuhakikisha kila mkenya anakuwa na maji safi, nataka kuona tunasonga mbele, sitakuwa mbele yaani nitakuwa Magufuli nawaambia” Alisikika Jaguar wakati akizungumza na wanachi wa Kibera.
Msanii huyo alipewa wadhifa huo juma lililopita katika hafla iliyo hudhuriwa na watu maarufu, miongoni mwao Waziri wa Maji, Eugene Wamalwa na Makamu wa Rais Nchini Kenya William Ruto.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi