Huko Twitter kumekucha baada ya Dada wa Waziri wa Rais Magufuli, kuandika ujumbe mzito na mkali sana katika Tweet yake moja huko Twitter, Mwanadada Mwamvita Makamba amedai yeye kama Mwekezaji binafsi katika tasnia ya Fashion ametapeliwa na Mbunifu wa Suti matata Bwana Sheria Ngowi. Ngowi anaesifika sana Africa nzima kwa ubunifu wa mitindo ya nguo mpaka kukubaliwa kumvika nguo Rais wa Zambia, anasadikiwa kumtapeli dada huyo wa Waziri wa Mazingira katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. January Makamba. Tweet hiyo ilisomeka kama ilivyo hapo juu na kuzua gumzo zito mitandao yote ya kijamii Tanzania kama kulikoni hasa?
sheria-ngowi
SHERIA NGOWI
mwamvita-makamba
MWAMVITA MAKAMBA
Hapo alikuwa akimpa taarifa jamaa anayeendesha kipindi kipya mjini cha Papo Kwa Papo na Papi kinachoruka kila jumatano saa 3 kamili usiku kupitia YouTube na kinakuwa Mubashara.