,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, December 1, 2016

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za kijiji hadi mkoa kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Lukuvi ametoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa ngazi mbalimbali katika mkoa wa Kigoma ambapo amesema mazoea ya kugawa maeneo bila kuzingatia vigezo ndiyo yamesababisha kuwepo kwa migogoro kila maeneo nchini na sasa ni jukumu la waliogawa kufanya kazi ya kuitatua katika kipindi cha mwezi mmoja.
“Viongozi wote wa mikoa na wakuu wa wilaya jukumu la kutatua migororo ya vijiji ni lenu kwasababu nyinyi ndiyo mliopendekeza vijiji vigawiwe, nyinyi ndio mliopendekeza kata zigawiwe na nyinyi ndiyo mliopendekeza vijiji na kata. Kwahiyo nendeni chini kule mkatatue na ningefurahi nchi nzima hii ifikapo tarehe 30 mwezi Disemba muende kwenye maeneo yote kwenye orodha yote mliyoisema ya migogoro ya vijiji mkatatue kwa kushirikiana na wale wananchi,” alisema Lukuvi.
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam katika ziara yake ya siku 10 jijini Dar es salaam amekuwa akikumbana na migogoro mingi ya ardhi katika mkoa wake.

BY: EMMY MWAIPOPO

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi