,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, May 15, 2017


Image may contain: one or more people

"ALIYEUAWA JANA NI JAMBAZI "
Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es salaam Simon Sirro amesema Mtu aliyeuawa jana ni Jambazi.

Jambazi huyo aliyekuwa na wenzake watatu waliokimbia walikuwa na Pikipiki mbili aina ya Boxer wakiifukuzia Gari la G4S iliyobeba fedha
Milioni 320 kupeleka kwenye ATM hapo Kurasini Makao Makuu ya Uhamiaji, Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Sophia Hussein...na ndipo walipotokea Majambazi hao Wanne na piki piki zao,..Jambazi huyu kabla ya kupigwa risasi aliruka kwenye pikipiki na kujaribu kumpora Silaha askari aliyekuwa akisindikiza Gari lenye fedha na askari wengine.


Kamanda Sirro anasema kwamba Majambazi yale hayakujua kwamba Gari la Fedha lilikuwa likisindikizwa na askari, Jambazi aliyepigwa Risasi amekutwa na Simu yake ya Mawasiliano, Hivyo Upelelezi unaendelea ili kuwapata Wale watatu waliokimbia na Mtandao wao Mzima.

Sirro - "Watu Wakae kimya na wasizungumze wasichokijua, Jeshi la Polisi linandelea na Uchunguzi wake, Jeshi halitamfumbia Macho Mhalifu yeyote anayetaka kutumia Silaha kuhatarisha Mali au Maisha ya Raia wengine, na Ndugu wasitumie Mwanya huo kuwalinda ndugu zao ambao ni wahalifu aidha kwa kujua au kutokujua"

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi