,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, May 15, 2017

MTU mmoja anayesaidikiwa kuwa ni jambazi ameuawa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika eneo la Kurasini, wakati yeye na wenzake wawili wakijaribu kupora fedha zilizokuwa zinapelekwa kwenye ATM ya benki.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana zilieleza kuwa majambazi hao walikuwa wakinyemelea kupora fedha zilizokuwa zikipelekwa kwenye mashine za kutolea fedha za benki ya CRDB tawi la Kurasini.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Simon Sirro, alitihibitisha kuwapo kwa tukio hilo alipozungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana.
“Ni kweli kuna tukio kama hilo, lakini taarifa kamili zitatolewa kesho baada ya kuzikamilisha,” alisema Kamanda Sirro, hivyo “kwa leo siwezi kuzungumza lolote. Nadhani unanielewa?”
Taarifa zilidai askari wa kampuni binafsi ya ulinzi ya G4S walikuwa wakipeleka fedha kwenye ATM Kurasini, lakini waligundua kuna pikipiki mbili zilikuwa zinawafuatilia.
Habari zilidai zaidi kuwa G4S walipokaribia tawi hilo la CRDB, majambazi yakaanza kuwashambulia kwa risasi, lakini askari wa FFU waliokuwa kwenye eneo hilo walijibu mapigo na kuua jambazi moja. Ilielezwa majambazi wengine walikimbia bila ya kupora fedha hizo.
Source: Nipashe

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi