,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, May 15, 2017

Mkali wa wimbo ‘Kiboko ya Mabishoo’ Harmorapa amemtaka Dogo Janja kuacha kujinadi kuwa yeye ni mkali wa kuvaa.

Rapa huyo ambaye wiki hii ameachia wimbo wake mpya ‘Nundu’ , amedai yeye ni mkali wa kuvaa kuliko hata mkali huyo  wa ‘Kidebe’ kutoka Tip Top Connection.
“Dogo Janja asijinadi sana kwenye kuvaa, mwambie tupo wanyamwezi kama sisi tunavaa pamba kali,” alisema Harmorapa.
Aliongeza, “ Najua na yeye ni mkali wa kuvaa lakini mimi ni mkali zaidi kwenye hizo, kwanza angalia jinsi nilivyotupia leo, kinyamwezi,”
Katika hatua nyingine rapa huyo amesema anamkubali sana Dogo Janja kwa kuwa ni msanii kijana ambaye amejaribu kufanya mambo makubwa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi