,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, May 16, 2017

Msanii kutoka PKP, Neddy Music amefunguka na kuwataka wasanii kutoka Zanzibar kuacha kulalamika kukosa usimamizi ndiyo chanzo cha kushindwa kufanya muziki wa bongo fleva na badala yake wajitume kuonyesha vipaji vyao ili kuwashawishi wadau wa muziki.

Nedy ameyatoa hayo ya moyoni leo kwenye Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kwamba siyo kwamba wadau wa muziki wa Zanzibar wameshindwa kuwekeza lakini wanaogopa kutoa pesa pasipo kuwa na uhakika kama mahali anapowekeza patamletea manufaa kwake na kuongeza kwamba vijana 
"Siyo kwamba Zanzibar hakuna wadau wakuendeleza muziki lakini wasanii je waliopo wameweza kuonyesha kitu walichonacho ili  kuwa prove wrong wadau. Unatakiwa kumshawishi mdau wa muziki akuone wewe ni dhahabu na akiweka pesa yake ajue haiwezi kupotea. Mara nyingi nikipata nafasi huwa nawashauri waweze kujionyesha uwezo wao na siyo kulalamika. Wewe usipojitangaza hakuna atakayeota kuwa wewe unathamani katika muziki na mimi ndipo nilipotokea kufanya kazi bila kukata tamaa"- Nedy Music.
Hata hivyo Nedy amefunguka na kusema kwamba suala la dini lisiwe kikwazo kwani muziki nao ni sehemu ya ajira hivyo kinachotakiwa ni wao wenyewe kutenga muda wa kazi na na muda wa kufanya ibada.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi