,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, May 15, 2017


Wastara Juma ambaye baada ya kutua Bongo akitokea nchini Sweden alikokuwa kikazi, anadaiwa kufulia na kushindwa kulipa kodi ya ile nyumba aliyodai kuinunua huko Ukonga, Dar.
ADAIWA KUJIPANGA KURUDI TABATA
Ubuyu mzito umeshushwa kwenye Wikienda kuwa, kwa sasa Wastara anajipanga kurudi kuishi kwa dada yake, Tabata, Dar alikokuwa akiishi zamani.
Mtoa ubuyu wetu alinyetisha kuwa, si kweli kwamba, nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Wastara kabla ya kutimkia Sweden aliinunua kama alivyodai badala yake alipanga na sasa ameiacha kwa sababu hali yake kiuchumi ni tete.
TUJIUNGE NA MTOA UBUYU
“Hivi mnajua kuwa ile nyumba ambayo Wastara alikuwa anasema ameinunua si kweli, alikuwa amepanga? Sasa imebidi arudi kwa dada yake, Tabata kwa sababu maisha ya kupanga yamemshinda,” alitonya mtoa ubuyu huyo kwa ombi maalum la kutotajwa gazetini.
WIKIENDA HALILAZI DAMU
Kama kawa, Wikienda huwa halilazi damu hivyo lilianza kuichimba habari hiyo ili kupata ubuyu mtamu ambapo lilimsaka Wastara na kufanya naye mahojiano juu ya ishu hiyo ambapo mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Mambo vipi Wastara? Tumepata ubuyu kuwa umerudi Bongo kutoka Sweden lakini inasemekana mambo si mambo. Hapa kuna ubuyu kuwa ile nyumba uliyosema umeinunua na kuimiliki maeneo ya Ukonga si yako. Pia kuna madai kuwa imekushinda kwa sababu umeshindwa kuilipia kodi, je, hili likoje?
Wastara: Dah! Jamani nimeamini watu ni wambeya sana. Mbona mimi nipo Ukonga? Ila ni kweli nina mpango wa kuhama, lakini ‘pliiz’ si mambo ya kodi. Huku (Ukonga) nilihamia kwa sababu ya mtoto wangu. Sasa amemaliza masomo hivyo nahama, lakini siyo kwamba nimekosa kodi. Siwezi kukosa ninyi wenyewe mnajua.
Wikienda: Vipi kuhusu suala la kuinunua nyumba hiyo?
Je, ni kweli kwamba hukuinunua maana suala hilo linaleta utata?
Wastara: Wewe elewa nilichokueleza, kuhusu nyumba, mimi nina nyumba tatu, nikiamua nikae ipi ni mimi ndiye ninaamua. Hakuna wa kunipangia.
Wikienda: Wastara mbona unakuwa mkali? Pia kuna habari kuwa kwa sasa unatembelea Bajaj na kwamba gari lako lipo juu ya mawe. Unalizungumziaje hilo?
Wastara: Mimi najua anayeeneza mambo yote hayo yote ya uongouongo ni kijana wangu wa kazi ambaye nimemfukuza juzikati kwa sababu ameniibia. Nimekuwa nikitendwa sana na vijana ninaowasaidia kazi kwa hiyo mimi sishangai, najua yatasemwa mengi juu yangu.
NENO LA MHARIRI
Kama kweli Wastara anasingiziwa tunampa pole na kumtaka kuwa makini na vijana wake wa kazi ambao amekuwa akiwalalamikia mara kwa mara kuwa huwa wanamfanyia mambo ya kihuni kisha kumwacha akiugulia maumivu.
NI TABIA YA BAADHI YA MASTAA
Hata hivyo, baadhi ya mastaa wamekuwa na tabia ya kudanganya juu ya misha yao halisi. Wamekuwa wakidanganya kuwa wanamiliki vitu vya thamani, lakini tunapozama kusaka ukweli huwa wanaumbuka na mfano mzuri ni nyumba aliyokuwa akiishi Wema Sepetu, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar ambayo mwanzoni alidanganya kuinunua ilihali alikuwa amepanga.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi