,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, May 19, 2017

Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi kuwa, Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji au muathirika kwa matukio yenye madhara mwilini, ajali au matukio yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi, ubakaji, kulawiti, kunywa sumu na mengineyo.
Ieleweke wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida kwa mujibu wa sheria, fomu hiyo inapaswa kutumika kwa kila tukio la aina tajwa hapo juu ili muathirika aweze kupata matibabu katika vituo vya Afya na hatua za kiupelelezi kwa Jeshi la Polisi ziweze kuendelea. 
Katika mazingira mengine hali ya muathirika inaweza kuwa mbaya, hivyo, huduma za kuokoa maisha (huduma ya kwanza) zinaweza kuendelea kutolewa wakati watoa huduma ya afya wakiijulisha Polisi ili kuharakisha upatikanaji wa PF 3.

Imetolewa na:-

Advera Bulimba-ACP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi