,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, May 19, 2017

W. J. Malecela

- Hahaha Ndugu najua unasoma hapa, naomba kukuhakikishia kuwa umedanganywa na huenda hujui kinachoendelea, halafu punguza chuki kwa RC hajakukosea chochote zaidi tu ya kurubuniwa kwako na wanaomchukia kwa sababu yupo karibu na Rais. Hao wanasiasa waliokurubuni huko waliwahi pia kukurubuni na kumbu kumbu zake zipo humu JF toka ulipokuwa unasoma London/UK, jana nimeona matusi uliyomrushia mwananchi mmoja huko kwenye Group lako la Watsap ambaye umemtukana sana kwa sababu ya kumuunga mkono RC, WHY? Mkuu RC wewe binafsi amekukosea nini hasa cha kukufanya wewe kutukana matusi ya ajabu vile?


- Kwa nini unasema Uongo kwenye huu waraka wako kama ule uongo uliousema kuwa RC alikukimbia ofisini kwake? Uongo wa kitoto ambao sikutegemea mtumzima msomi kama wewe unaweza kujiingiza nao, Ofisi ya RC ina Milango Miwili mmoja wa kuingilia na mwingine kutokea kwa pembeni kwa hiyo hakuna Mlango wa nyuma kama ulivyodai ulikuwa ni uongo wa kitoto sana, na besides ili umfikie RC ofisini kwake ni lazima upitie Getini ujiandikishe wamuulize Secretary wake ndio uruhusiwe kupanda juu kwa Secretary wake usubiri amfahamishe RC kuwa upo ndio uruhusiwe kuingia kumuona, sasa kama RC alikuwa hataki kuwaona na Tume yako hivi kweli alihitaji kuwaruhusu mfike mpaka ndani ya ofisi yake ndio akimbie? Huoni kuwa ni uongo wa kitoto wakati unajua kabisa siku mliyopanga kwenda kumuona ndiyo siku Bosi wake Waziri wa Tamisemi alimpitia na kwenda naye Ilala Machinga Complex, sasa wewe uliendaje kumuona RC ambaye hakuwepo ofisini I mean WHY UNADANGANYA?

- Leo again umeibuka na uongo mpya kwamba eti kuna "Wpambe wa RC wanaojaribu kuwaomba Waandishi wamuandike" ...hahahahah kwanza naomba kucheka sana kwa sababu binafsi nimefuatwa na kundi la Waandishi walionifahamisha kwamba wana mpango wa kuachana na mgomo wako na kuanza kumuandika kwenye magazeti yao 5 makubwa hapa mjini, na wakaniomba nimfahamishe RC ili awakatie mzigo hahahahaha niliwacheka sana nikawaambia kwamba HAITAKUJA KUTOKEA NEVER maana kwa maneno mengine walichokitaka inaitwa "BLACKMAIL" niliwauliza so mligoma ili mje mdai pesa kumuandika? hahahahahahha

- Mkuu wewe, ni mtu unayetakiwa kuheshimika na jamii kwa usomi na kazi yako lakini kwa kukubali kutumiwa na Wanasiasa umejiharibia sana na kwa muda mrefu sasa, I mean hizi Chuki zako na wanaokutuma zitawasaidia nini hasa mbele ya Wanasiasa ambao hubadilika kila siku? Majuzi Lowassa alikuwa adui namba moja wa Wanasiasa wa CCM wanaokutuma leo ni Rafiki yao mkubwa kwa siri tunajua sana. So how can you trust your life kwa Wanasiasa wa namna hiyo ambao Mange alikuwa adui yao mkubwa leo ni Rafiki yao mkubwa mpaka wanampa habari nyingi za uongo kama za Kinana au mnadhani hatufahamu? Tunajua sana ila tunajiuliza mnachopigania ni nini hasa wakati Uchaguzi ulishaisha Mwaka 2015?

- Nikukumbushe tena hakuna Mwandishi aliyeombwa kwa kushawishiwa kupewa rushwa ili amuandike RC hapana, ila kuna Mjumbe wa hilo Baraza lako aliyemtishia sana Muandishi atakayemuhoji RC Jumatatu hahahahaha naomba kukuambia kwamba huo muungano wenu ni wa wachawi hauwezi kudumu ndio maana tulisema it is about time tu mtavurugana wenyewe kwa wenyewe, kwa sababu magazeti sasa hivi hayauzi na tunajua kuna Wanaowalipa kufidia hasara lakini hata wao wanawalipa kwa taabu sana hahahahaha anyways nakuomba usijiaminishe sana kuandika kama unawaongoza Waandishi wote HAPANA, maana wengi wanahangaika na njaa na huu mgomo. Wewe na wanaokutuma mlishashindwa siku nyingi na mtashindwa tu maana hamna sababu ya msingi ya mgomo na hakijaharibika kitu cause slogan yetu ni ile ile "KAZI JUU YA KAZI yaani BAMPA TO BAMPA". Halafu jitahidini basi Jukwaa lako na Wanasiasa wanaokutuma mfanye kitu cha msingi kwa jamii kama RC anavyofanya, Jengeni Mahospitali tu kusaidia Wananchi ili tujue kwamba umoja wenu ni wa nguvu kama ulivyosema sio wa kujitokeza kutaka kumchagulia Rais viongozi wake hahahahaha

- By the way hii interview itafanyikwa Jumatatu Saa Moja na Nusu Asubuhi, Tarehe 22/5 unakaribishwa sana kuhudhuria au kuangalia kwenye Luninga wa Star TV, otherwise nimejifunza kwamba kumbe kupigana na Wauza Madawa ya Kulevya sio mchezo maana majibu yao ndio haya tunayaona kwa macho yetu sio tena kwa kusimuliwa! Nakukumbusha sana kwamba mgomo wakomunawaumiza sana Waandishi wa Habari wasiolipwa Mishahara kwa muda unaotakiwa, wasiokuwa na pensheni wala Bima za afya, jitahidi basi kuwapigania kwenye hayo na hilo Baraza lako msiishie kumgomea RC tu!

- Kuhusu mnaouita "UVAMIZI WA CLOUDS" naomba kusema tena na tena nimeamua kuunyamazia kwa sababu Mmiliki wa Clouds ni rafiki yangu waa karibu sana ndio maana sipendi kugusa hiyo ishu, ambayo ninajua ilivyopangwa kwenye vikao huko Dodoma na washiriki wote wa hivyo vikao tunawajua, ni aibu tupu kwa watuwazima kutishiana nyau kwa ishu ambazo mnajua kabisa kuwa ni uongo wa kitoto sana ila endeleeni kuwadanganya wasioelewa.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

- Le Mutuz Nation
 
UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

Deodatusi Balile
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
Mei 19, 2017

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi