,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 20, 2017

 Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano.
 Kijana mmoja, Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano alizokuwa amezificha ndani ya mapande ya nyama yaliyorostiwa.
Tukio hilo la ajabu limetokea jana baada ya Nomba kuwapelekea ndugu zake chakula.

Mfano wa simu alizokamatwa nazo Ramadhan Nombo
Kwa mujibu wa chanzo, Nombo alipanga kuingiza simu tano ambazo alizipachika kwenye mapande ya nyama iliyorostiwa kisha kuwapelekea ndugu zake walioko gerezani hapo.  Hata hivyo, haikufahamika alikuwa anawapelekea kwa sababu gani, na wafungwa wa kesi zipi.

Mtandao huu ulimtafuta Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, ASP Lucas Mboje ili kuzungumzia tukio hilo ambapo alikiri kutokea na akaelekeza aonwe Mkuu wa Magereza wa Dar.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP Augustine Mboje alipoulizwa alisema ni kweli kijana huyo amekamatwa.

Kama akikutwa na hatia atakuwa amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria za Magereza sura ya 58 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, inakataza kwa mtu yeyote kuingiza kitu chochote kisichoruhusiwa gerezani na atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita(6) au faini au vyote kwa pamoja.
Hadi sasa Nombo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi