,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, June 15, 2017

Image may contain: text
Benki kuu ya Tanzania (BOT) imepiga marufuku mchezo wa upatu ujulikanao kama D9. Taarifa iliyotolewa na BOT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) inasema mchezo huo ni haramu na ni kinyume na sheria ya makosa ya jinai sura ya 16.
Hii ni kusema kuanzia sasa kile kilichoitwa D9 kimekufa rasmi. Mtu yeyote atakayeonekana kujihusisha na mchezo huo atachululiwa hatua za kisheria.
Nimekumbuka nilivyoshawishiwa kujiunga kwenye mchezo huo kwa kigezo cha kupata hela "chapchap". Sikushawishika kabisa maana najua principle ya kupata hela ni lazima uitolee jasho. Katika ulimwengu huu wa "kibepari" hakuna pesa inayopatikana bila kufanya kazi.
Bahati mbaya kuna watu waliajiingiza kwenye mchezo huu kwa kushawishiwa na watu wanaowaamini. Wengine wakajisajili wao na familia zao. Mtu kajisajili yeye, mke na watoto. Kila mmoja kalipa dola 2000+, akitegemea kuvuna dola 170 kila wiki. Leo mchezo huo unapigwa marufuku halafu alikua hajavuna hata mara moja. What a mess.!
Ni vizuri tukawa makini na hizi biashara za mtandaoni. Usije kuinvest pesa yako bila kupata taarifa sahihi juu ya biashara husika. Mnakumbuka DECI?? Nayo ilikua hivihivi. Poleni wote mliopoteza fedha zenu kupitia D9.!

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi