,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, June 19, 2017

Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimesema hakitokubali kubaki na wanachama wasaliti na kitahakikisha kuwa kinawatimua ili uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kuchukuwa majimbo yote visiwani humo .

Naibu katibu mkuu wa chama cha (CCM) Zanzibar, Dkt.Abdullah Juma Saadala (Mabodi)Msimamo huo umetolewa na Naibu katibu mkuu (CCM) Zanzibar, Dkt.Abdullah Juma Mabodi wakati akizungumza na wanachama wa CCM wa umoja wa wanawake wa mkoa wa mjini Magharibi ambao wanashiriki mafunzo ya uongozi ambapo amesema yeye nafasi aliyopewa ya ukatibu ni kuhakikisha anafanikisha lengo hilo.

Mtendaji huyo mpya wa (CCM) amesema sasa ni wakati wa kusafisha chama na kuwaondoa wasaliti wa chama hicho ili kubakiza wanachama ambao ni wazalendo na waonajua chama kinataka nini.

Mapema mjumbe wa kamati kuu ya CCM na mbunge wa kuteuliwa, Khadija Hassan Aboud amewataka akina mama nao kuanza kujiendeleza kitaaluma ili kupata nafasi ya kukiendesha chama hicho kwani nwanawake wana ushawishi mkubwa kwenye jamii.

Mafunzo hayo ya siku moja kwa Wanachama wa ( CCM) watapata fursa ya kujiendeleza kitaaluma na uongozi na kufahamu misingi ya uongozi unavvotakiwa ndani ya chama kulelekea uchaguzi mkuu 2020.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi