,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, June 11, 2017

Hatimaye fainali za michuano ya SportPesa Super Cup  zimemalizika jioni ya leo huku timu ya Gor Mahia kutoka Kenya ikuchukua ubingwa baada ya kuitandika AFC Leopard kwa mabao 3-0 katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Kwa ushindi huo Gor Mahia inajinyakulia zawadi ya dola elfu 30 ($ 30,000) huku ikisubiri kuja kucheza na Everton ya nchini Uingereza July 13 jijini Dar es salaam.
Mchezo huu umeifanya Gor Mahia kuvunja rekodi waliyojiwekea wenyewe  katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Sportpesa kwa kuwa timu iliyoongoza kupata magoli mengi kuliko  timu zote zilizoshiriki michuano hiyo huku ikikomaa kumaliza michezo yake ndani ya dakika 90 uwanjani.
Ushindi wa Gor Mahia umetangazwa na wachezaji watatu walioweza kutingisha nyavu za mashemeji zao ambao ni Otieno Timothy, Oliver Maluba na John Ndirangu, huku mchezaji  Medie Kagere akichukua kiatu cha mfungaji bora wa michuano hiyo.
Kwenye michuano hii Gor Mahia imeonyesha ubabe wake ambapo tangu ilipoanza Jumatatu ya wiki hii imeweka kwapani goli saba bila kukubali kufungwa na timu zote walizokutana nazo.
Gor Mahia wakishangilia ushindi wakiwa na Kombe lao

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi