,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, June 17, 2017

Na Magreth Kinabo. Mahakama ya Tanzania.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, amewataka wanasheria wa Tanzania Bara kujifunza uzoefu wa kubadilisha sheria mbalimbali kwa kutumia vitabu vya sheria kutoka Zanzibar kwa ajili ya kufanya utafiti na kufundisha katika vyuo vikuu.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16.06.2017, na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wageni kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, wakati akizungumza na ujumbe huo mara baada kuwasili katika Ofisi ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo jijini Dar es kwa ajili mazungumzo ya kubadilisha uzoefu juu ya mabadiliko ya vifungu vya sheria mbalimbali.
Ugeni huo, ulikabidhi seti ya vitabu vitano vilivyobadilishwa kutoka 35, ambapo ulizungumzia kuhusu mabadiliko hayo na masuala mbalimbali ya Mahakama ya Tanzania.
“Kuna haja ya kujifunza sheria bora kutoka Zanzibar, ambazo zinaweza kusaidia kufanya tafiti mbalimbali na kutumika kufundisha kwenye vyuo vikuu.,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Aidha Mhe. Jaji Kaimu Jaji Mkuu huyo aliushukuru ugeni huo, kwa kukabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,Mhe. Omar Makungu.
Akizungumzia kuhusu vitabu hivyo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee Haji alisema vitabu hivyo vilivyokabidhiwa ni mabadiliko kutoka vitabu vya sheria 35 hadi vitano. Mabadiliko hayo ya kisheria yamefanyika kutoka mwaka 1980 hadi 2015.

Mhe. Mzee alisema ofisi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano na kubadilisha uzoefu wa masuala hayo na mengine ya Mahakama baina ya pande hizo mbili.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi