,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 20, 2017

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya kuwafikisha mahakamani, Habirnder Seth Singh na James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi baadhi ya viongozi wameweza kuandika jambo kuhusiana na watu hao kufikishwa Mahakamani.
Naibu Waziri wa Afya Mandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ametwee hivi:
Mshahara wa dhambi ni mauti. Hakika hakuna marefu yasiyo na ncha. Leo Ndg. Harbinder Singh Sethi na Rugemalira wako mbele ya jicho la sheriaLeo vita dhidi ya ufisadi, uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi imepata sura mpya.
Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe nae katweet kuhusu tukio hilo huku akiweka picha za wahusika hao.
Leo ninaona vita dhidi ya ufisadi Ina maana kubwa. Kumkamata Harbinder Singh Seth na kumfikisha mahakamani ni hatua kubwa ya kupongezwa Rais Magufuli nimekuwa nakupinga kwenye mambo mengi, na nitaendelea kukupinga, lakini kwenye hili la IPTL umetendea nchi haki. Hongera Sana Leo Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari alisema leo wamewafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, kwa makosa ya kuhujumu uchumi ambao ni Habirnder Seth Singh na mfanyabiashara James Rugemalira.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi