,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 20, 2017

 
 Mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chama cha Demokrsia na Maendeleo (CHADEMA), Mwita Waitara  leo bungeni ameamriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoka nje ya bunge hilo kwa madai kuwa alikuwa akibishana na kiti cha Spika.

Waitara alitolewa nje ya bunge baada ya kuomba muongozo kufuatia kauli aliyotoa Spika wa Bunge kuwa wabunge wote wanaoikataa bajeti hiyo wanakataa maji na maendeleo jimboni kwao.  
"Waitara sitaki miongozo, nakuomba ukae chini, Waitara nakupa onyo la kwanza, masanjeti wa bunge anzeni kukaa sawa, naomba askari ya bunge mkae sawa sawa popote pale mlipo, wewe unayeongea nakuomba utulie wenzako waongee, wewe Katibu anayenijibu ni nani? Ni huyo huyo Waitara? Basi nakuomba Waitara utoke nje ya bunge sasa hivi kwa hiyari yako mwenyewe kabla sijaita wale mabwana wakubwa, nakuomba utoke nje haraka unanipotezea muda" alisema Spika Job Ndugai 
Kufuatia amri hiyo ya Spika wa Bunge Job Ndugai, Mbunge Mwita Waitara alitoka nje ya bunge mwenyewe bila tatizo lolote  
 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi