,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, June 13, 2017

Msanii wa Bongo Fleva na hit maker wa wimbo wa One Day, Nandy amesema Dully Sykes ni miongoni mwa wasanii ambao wanakubali kile anachokifanya kwenye muziki.

Muimbaji huyo ambaye mwanzo alikuwa akifanya kazi na Dully, alidhaniwa huwenda haelewani na mkongwe huyo ambaye pia ni producer wa muziki.
“Yupo sana proud na mimi kila tukikutana huwa ananisisitiza kuwa na heshima, kusikiliza wakubwa walionitangulia, kufanya kazi kwa bidii kwa sababu hustling yangu aliiona toka way back na ndoto zangu anazijua nyingi sana,” Nandy ameimbia Planet Bongo ya EA Radio.
“Kwa hiyo kaniambia ndoto zako zimetimia, so usiachia hiyo chance kwako kwa kufanya lolote baya.” ameongeza.
Katika hatua nyingine Nandy ameeleza yale maneno yaliyokuwa yanamuandama kuwa anamuiga msanii mwenzake, Ruby kwa sasa yamepungua kwani watu wameshajua na kuamini Nandy ni msanii wa aina gani.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi