,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, June 15, 2017

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection, Madee amesema mafanikio aliyoyapata kupitia wimbo wa Hela ni makubwa, huku akiwataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio mpya.

Wimbo wa Hela unaoendelea kufanya vizuri kwa sasa, Madee hajaweka wazi kiwango cha fedha kilichoingizwa na wimbo huo zaidi ya kusema umemuongezea mashabiki wapya.
“Hela ni wimbo ambao ni mkubwa umenipa mafanikio mengi, na nimeongeza idadi ya marafiki, mashabiki na nimepata hela nyingi lakini kiukweli sijui imeingia kwenye nafasi gani kwa sasa hivi ila nachojua nimeongeza wigo wangu kwa sababu ni wimbo ambao nimekuja nao katika viwango vya tofauti kabisa,” Madee ameimbia Dj Show ya Radio One.
Hata hivyo Madee ameongeza kuwa bado kuna ngoma nyingine kubwa inakuja ambayo ameshirikiana na msanii mkubwa barani Africa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi