,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, June 17, 2017

Msanii anayechipukia vizuri sana kwenye game ya Bongo Fleva Mrap Lion amefunguka kwa kusema uongozi wake haugopi kuwekeza pesa nyingi kwenye kipaji chake kwa sababu ya jitihada alizo nazo na alizokuwa nazo awali kabla hata ya kupata uongozi.

Mrap amefunguka hayo ndani ya Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kuwa kabla ya kupata uongozi 'Mukii International' alishakuwa na jitihada za kuhitaji kufika mbali, lakini uongozi alioupata  umekuja kumsaidia kutimiza malengo na kwamba hata uwekezaji wanaoufanya ni kutokana na juhudi anazoonyesha
"Ni kweli mimi ni mchanga lakini nina malengo makubwa sana. Nawaza kimataifa zaidi ndio maananajitajhidi kufanya kazi nzuri. Uongozi wangu hautupi pesa bure, nikwa sababu wana imani na mimi kwamba kuna kitu ndani yangu. nakumbuka  video yangu ya kwanza 'hawajui' nili hustle sana mpaka ikakamilika na ilikuwa nzuri japo ubora sityo wa kutosha , lakini kwa sasa nipo chini ya uongozi nafanya kazi kwa kujituma sana hata ratiba yangu ya kuamka imebadilika n, natia bidii mno ndiyo sababu wameamua kuweka hela ya kutosaha kwangu na mimi nawaahidi sintawaangusha" alisema Mrap.
Chini ya uongozi wa Mukii International Mrap amesha achia ngoma mbili ambazo ni 'Its not too late' aliyomshirikisha Mayunga pamoja na hii ya sasa aliyoichia wiki hii 'So Higher'

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi